Saturday, 14 September 2013

Hii ni kali ya mwaka .......Alawitiwa kwa kulinda ajira!

MDOSI au Kanjibai aliyefahamika kwa jina moja la Milah ambaye ni bosi wa kampuni moja ya ujenzi yenye makao yake Mwenge jijini Dar alinaswa chooni akiwa na mfanyakazi wake, John Carlos ‘Shabani’ (watu walimpachika jina la Shabani kutokana na Kanjibai wa kwenye Komedi) ikidaiwa walikuwa katika mazingira ya ulawiti, Ijumaa ‘Kubwa’ lina sinema yote. Ishu hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wawili hao walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia usumbufu watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.

KISA KILIPOANZA

Siku hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers, Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo. Alisema:

“Jamani hebu njooni haraka hapa kwenye hii kampuni ya ujenzi ya… (jina lipo) iko hapa Mwenge. Kuna bosi wetu mmoja amejifungia chooni na mfanyakazi mwenzetu kwa zaidi ya robo saa sasa, sijajua nini kinaendelea humo ndani. Sisi wengine hapa matumbo ya kuendesha yametushika sijui tufanyaje?!”
Mtoa habari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuwaambiwa mapaparazi wetu waliompokelea simu wachukue Bajaj au Bodaboda ili kuwahi.

Sosi huyo kabla ya kukata simu aliweka wazi ramani ya kufika kwenye choo hicho na kusisitiza kwamba muhimu kuwahi kwa sababu huenda wanagombana.

MAPAPARAZI WAWASHA PIKIPIKI

Kufuatia msisitizo huo, mapaparazi wetu makini  waliwasha pikipiki zao, kila mmoja na yake na kushika njia kuelekea eneo la tukio.
Hata hivyo, kwa kuamini wanaweza kukutana na lolote, waliona ni vyema kwanza kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge ambapo walipewa askari wawili kuelekea eneo la tukio.

ENEO LA TUKIO SASA

Timu hiyo iliwasili kwenye eneo la tukio. Mlango wa choo hicho ulikuwa umefungwa lakini kwa mara moja tu haikuwa rahisi kugundua kama ulifungwa kwa funguo au kawaida tu.
 Afande mmoja alijitolea kugonga mlango wa choo hicho ili kupima ushirikiano utakaotolewa na wawili hao au mmoja wao.
Sauti iliyoonekana ni ya Kanjibai kutokana na kushindwa unyoofu wa lugha ya Kiswahili ilisikika ikiuliza:
“Nani wewee… taka nini huku?”

Afande: Sisi ni askari polisi, fungua haraka tunajua mko wawili humo ndani, fungua.

Kanjibai: Subiri kidogo.
Baada ya dakika kadhaa ambazo mapaparazi wetu hawakuzifuatilia, mdosi huyo alifungua mlango na kukutwa akiwa na ‘Shabani’.

WALICHOKUWA WAKIKIFANYA CHOONI

Katika maswali ya harakaharaka nje ya choo hicho kila mmoja alisema la kwake ambalo aliliamini linaweza kumchomoa kwenye skendo hiyo mbaya.
‘Shabani’ alisema yeye aliingia kwenye choo hicho baada ya kuitwa na bosi wake huyo ambapo alishindwa kumkatalia kwa kuogopa kupoteza ajira yake na kama inavyojulikana maisha ya Dar bila kazi ni ngumu kuyamudu.

Alipoulizwa walichokuwa wakikifanya ndani ya choo hicho, Shabani alibaki akiwatumbulia macho maafande, wakati mwingine mapaparazi wetu.

Kwa upande wake Kanjibai alipotakiwa kujieleza kisa cha kuingia chooni na mfanyakazi wake, alisema alimuomba wazame humo ili akamnyoe. Yaani Kanjibai alitaka kunyolewa.

IKAFIKA ZAMU YA KUPELEKWA KITUONI

Afande mmoja aliamuru wawili hao wapelekwe kituo cha polisi, lakini kabla ya kuanza safari, mdosi huyo aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali na kutoa vitu vyake kadhaa na kuwakabidhi wadosi wenzake waliofika ‘kumsaidia’ muda mfupi baada ya kunaswa.
Halafu aliingiza mkono kwenye mfuko mwingine na kutoa mafuta aina ya KY (pichani) ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’ lakini askari alimwambia mafuta hayo yanatakiwa kituoni kwa ajili ya ushahidi hivyo asiwape nduguze.
Breki ya kwanza ilikuwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mwenge ambapo baada ya mahojiano mafupi walihamishiwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ ambapo walihojiwa zaidi kuhusiana na tukio hilo.


Angalia picha za tukio hapa chini
...Choo walipokuwa wamejifungia Milah 'Kanjibai' na John Carlos ‘Shabani’.

...Ndani ya choo walimokutwa.

...Mafuta aliyokutwa nayo Kanjibai ambayo mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’.

...Wakiwa chini ya ulinzi.

Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • NGASSA akata Mzizi wa Fitina...... atua Mazoezini Yanga HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), amekata mzizi wa fitna baada ya kuanza kujifua rasmi na timu hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe. Awali kulikuwa na utata wa mchezaji huy… Read More
  • Wema Sepetu matatani tena? DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa h… Read More
  • Dida apigwa dongo BAADA ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’ kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza na Ijumaa kwa… Read More
  • JOHARI: SITEGEMEMI MABUZI KAMA MASTAA WENGINE   STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa hategemei wanaume kama wanavyofanya mastaa wengi wa kike Bongo.Akipiga stori na paparazi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Johari amewataka… Read More
  • Soma habari kamili ya Bibi Harusi aliyeaga dunia dakika 30 kabla ya kufunga ndoa Bi harusi huyo, Levina Mmassy (23) aliyekuwa mkazi wa Chanika, Handeni mkoani Tanga alifariki dunia Jumamosi ya Julai 6, mwaka huu, majira ya mchana, muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Kasisi Masawe. PADRI ASUBIRI Tuki… Read More

0 maoni: