Habari zenu Wana hot n Town!
Ni masikitiko na majonzi kwangu na kuumia sana moyo...maana nilitokea kupendana sana na binti mmoja wa kisukuma na hata kutambulishana kwa familia zetu...mwaka jana nimebahatika kupata nafasi ya masomo nchini Afrika Kusini...na mwaka huu niliporejea nchini nimemkuta mchumba wangu tayari ni mjamzito wa miezi mitano...maana nilirudi tu bila kumpa taarifa kuwa narudi kwa likizo, na hapo alihamaki sana kuniona ghafla nyumbani kwao...tayari akiwa na tumbo kubwa.
Basi baada ya salamu na kumuomba kwa upole tutoke ndipo akanisimulia mkasa wote kuwa amepata mimba na muhusika ni mume wa mtu ambaye ni mfanyakazi mwenzake ofisi moja. Binti analia na kuniomba msamaha kwa lililotokea na anataka tuendelee na mipango yetu ya awali. Sikutaka kumwambia chochote zaidi ya kubaki na mshangao wa tukio zima na kuona kama movie ya kibongo.
Wadau kiufupi nipo katika msongo mkubwa wa mawazo na hasa aibu kwa wazazi wangu ambao walimpenda sana huyu binti na kuona ni hazina ya mke mwema katika maisha yangu. Nawakilisha kwenu wadau kuomba mawazo na uzoefu wenu katika hali ya namna hii...
Uncle L
0 maoni:
Post a Comment