Friday, 5 September 2014

Okwi: Nitacheza Simba hata bure


BAADA ya kufanikiwa kutua Simba, kiungo mshambuliaji mpya wa kikosi hicho, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa yupo tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo bure.

Okwi amesema maneno hayo akimaanisha kuwa yupo tayari kucheza bila hata kulipwa mshahara kwa kudai kuwa hilo suala la fedha siyo tatizo kwake.


Akizungumza na Championi Ijumaa, jana, Okwi ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga na kusaini kuichezea klabu hiyo kwa miezi sita, amesisitiza kuwa anaipenda Simba na atafanya hivyo pia itakapobidi ili kulinda kiwango chake.

“Unajua sasa hivi nimebadilika na siyo Okwi yule waliyekuwa wakimjua, sitakuwa mtukutu kama ambavyo walikuwa wakinisema mwanzoni,” alisema Okwi.

Mganda huyo ameongeza kuwa anaamini yuko mahali sahihi, hivyo atahakikisha anapambana kuweka kiwango chake kuwa bora. “Nimefurahi kurejea Simba na kuitumikia timu hii, mshahara siyo tatizo,” alisema Okwi.

Kwa hisani ya Martha Mboma/GPL

Related Posts:

  • OMMY DIMPOZ aponda ushirikina? Baada ya taarifa kuenea katika mitandao kuhusu Diamond anatumia mganga wa jadi katika kazi zake za muziki. Leo kupitia Clouds Fm double XXL katika jiwe la wiki rafiki yake wa k… Read More
  • Mpoto kugombea Ubunge? Mkali wa muziki wa ngonjera Tanzania Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba  amefunguka na kuweka wazi nia yake ya kugombea UBUNGE mwaka 2015. Mpoto amesema atagombea ubunge ila hajaweka wazi CHAMA  wala JIMBO atalogombea .… Read More
  • Bob Junior afunguka kuhusu kuoa mapema Msanii maarufu wa muziki wa  kizazi kipya almaarufu kama Bob Junior ambae pia ni mtayarishaji wa muziki amefunguka kuhusiana na sababu ya yeye kuweza kuchukua uamuzi wa kuoa mapema. Mr. Chocolate Flavour alifung… Read More
  • Wema haishi kwa vituko? arusha picha ya kimahaba na ujumbe mzito .... STAA wa filamu mwenye jina kubwa Bongo, Wema Abraham Sepetu, juzikati alitupia picha yake akiwa kimahaba zaidi na mwanaume aliyedai kuwa ni ‘mume’ wake.Picha hiyo ambayo aliiweka kwenye mtandao wa BBM inamuonesha msanii hu… Read More
  • Ndoa ya Aunt Ezekiel imekufa? KUMEKUWEPO na vijineno vya chinichini kuwa eti ndoa ya msanii maarufu wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel aliyofunga hivi karibuni na Sunday Demonte haipo na wabaya wake wamekuwa wakieneza taarifa hizo kwa kasi ya ajabu. Wa… Read More

0 maoni: