Friday, 21 June 2013

Bongo bwana? Urafiki wa WEMA na KAJALA kwishney? wapambe ndio chanzo.......

KIMENUKA! Utabiri wa wengi kuwa ushosti wa waigizaji masistaduu wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja kutumbukia nyongo unadaiwa kutimia na sasa wametibuana, Ijumaa limenyetishiwa. Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu (jina linahifadhiwa), mwanzoni baada ya Wema kumlipia Kajala faini ya Sh. milioni 13 na kumnusuru kutokwenda Segerea a.k.a Segedansi, wawili hao walikuwa marafiki kama pete na kidole.
SIKU KAMA HIZI

“Walishinda wote, walilala wote, walikwenda klabu wote yaani Kajala alikuwa anamnyenyekea ‘madam’ Wema kwa kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela,” kilisema chanzo chetu na kuongeza: “Kuna wakati hapa katikati Kajala alikuwa kama katibu muhtasi wa madam, si unajua lazima atumikie fedha za watu? “Kabla hajaenda Mwanza kwa ajili ya mapumziko kwa bibi zake, nilimsikia Kajala akilalama kuwa madam aliamka siku moja akawa amemchunia, unaambiwa hata salamu ikawa hakuna.

TATIZO NI WAPAMBE

“Hapo ndiyo maneno ya pembeni yakaanza kwa sababu mbali na Kajala, Wema pia ana wapambe wengine na mbali na Wema, Kajala naye ana kampani. Kwa hiyo sosi ya manenomaneno ni hizo kampani zao. “Ipo siku kabisa Wema alimlalamikia Kajala hadharani kuwa amekuwa akimsema vibaya kwa watu. “Yale maneno yalimuuma sana Kajala, ikabidi arudi nyumbani kwao lakini akawa anaogopa kumwambia mama yake kuwa ametibuana na Wema hadi alipotimkia Mwanza.

KUMBE ALIMKOSESHA DILI?

“Lakini kabla ya hii ishu ya kulaumiana, kipindi cha nyuma kidogo Kajala alipata dili la kwenda kurekodi filamu nchini China na mastaa wengine lakini ikadaiwa kuwa Wema alichomoa hivyo mwigizaji huyo hakwenda pamoja na kwamba alishapewa baraka zote na baba yake. “Unaambiwa alikuwa amekamilisha taratibu zote za kwenda China, hadi tiketi alikuwa ameshakata lakini suala hilo lilipotua kwa Wema, ilidaiwa kuwa alikataa kumruhusu.

TATIZO MILIONI 13?

“Mimi nakwambia zile milioni 13 zinamkosesha raha Kajala hadi unamuona kabisa kwamba ana stress (msongo wa mawazo).  “Wewe fikiria, kazi inayomwingizia mkwanja ni filamu, sasa unaambiwa inadaiwa kuwa madam hataki acheze filamu za watu wengine, sasa ataishije jamani?

SASA NI KUNUNIANA KWA KWENDA MBELE

“Mimi nakwambia ndiyo maana ameamua kwenda kupumzika Mwanza baada ya kuwa wananuniana kwa kwenda mbele.” Baada ya kupata habari hizo, Ijumaa lilimtafuta Wema kwa njia ya kilongalonga chake cha kiganjani ili kupata undani wa sakata hilo lakini hakupatikana hewani.

NYUMBANI KWA WEMA

Baadaye mwanahabari wetu alisaga lami hadi kwa staa huyo Kijitonyama, Dar, alipogonga geti alitoka mlinzi aliyedai kuwa ‘malkia’ alikuwa ndani amelala na hakuhitaji usumbufu pamoja na kwamba ilikuwa saa 6:30 mchana.

MENEJA WAKE ANASEMAJE?

Hata hivyo, Ijumaa lilibisha hodi ofisini kwa Wema, Mwananyamala-Komakoma ili kuzungumza na meneja wake, Martin Kadinda ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Kajala yupo Mwanza, aliomba ruhusa ya kwenda kupumzika tukampa. Hayo mengine ya kutibuana na madam siwezi kuyasemea kwa sababu yapo nje ya uwezo wangu. “Lingekuwa ni suala la kazi hapo sawa lakini ni vizuri ukazungumza na mkurugenzi mwenyewe (Wema) lakini sidhani kama ataweza kuzungumza kwa sababu alikuwa anaumwa, amezidiwa na kupelekwa hospitali.”

WEMA ANAUMWA NINI?

Alipoulizwa Wema anaumwa nini, Kadinda alifunguka: “Sijajua lakini ugonjwa ni siri kati ya mhusika na daktari, cha msingi wewe ujue tu anaumwa.”

HUYU HAPA KAJALA

Baada ya kupita kote huko kusaka undani wa sakata hilo, Ijumaa lilimgeukia Kajala kwa njia ya simu ya mkononi akiwa jijini Mwanza na kumuuliza kulikoni kutibuana na Wema. Huku sauti ikiwa chini, Kajala alisema: “Ni kweli kuna hali ambayo hata mimi mwenyewe nashindwa kuelewa lakini siwezi kuzungumzia kwa leo nikiamini yatapita.”


Habari na Musa Mateja wa GPL

Related Posts:

  • Fumanizi la LULU, YOUNG DEE utata MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa n… Read More
  • Mwalimu afa kimiujiza Mwalimu Gloria Tarimo ‘Ticha Gloria’ (29) aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Mbezi High School ya jijini Dar, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakidai kifo chake ni… Read More
  • Penzi la AFANDE SELE na MAMA TUNDA kwisha? Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Shiengo ‘Mama Tunda’, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani. KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi ‘Af… Read More
  • Baby Madaha afunguka .....watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao STAA wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe. Akipiga stori na paparazi… Read More
  • Aishi kwenye handaki kwa miaka minne DUNIA haiishi vituko! Chacha Makenge (36) mzaliwa wa Kijiji cha Kisangula, Mtukula, Serengeti mkoani Mara anaishi jijini Dar lakini ndani ya handaki aliloligeuza chumba kwa miaka minne sasa, ni ajabu lakini ni kweli. … Read More

0 maoni: