Friday, 26 April 2013

Diamond aishi vituko asema .... Naenda LONDON kumletea Mama Mchumba

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.


Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.
Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.


Kwa hisani ya - GLP

0 maoni: