Thursday 30 May 2013

Silaha Wanazotumia wanawake wanapojihami

Wanawake wengi wanapokosa na  kuhisi kuharibu hutumia silaha hizi kama ngao ya kujihami kwa wenza wao

MACHOZI
Hii ni silaha ambayo mwanamke amejaliwa.Baadhi ya wanawake wanapotaka kufanikisha jambo kwa mwanaume basi ushawishi wao hudhihirishwa kwa machozi.Haya huyafanya anapojitetea kuwa yeye hakufanya jambo fulani .... mfano Wenye wachumba pia hudaiwa na machozi ya mwanamke ili kuficha ukweli uhusiano usiishe.
MENO
Hii ni silaha ambayo mwanamke akiamua kuitumia hasa anapokuwa mazingira hatarishi.Mwanaume hata awe baunsa kiasi gani,hawezi kumlazimisha kimapenzi mwanamke ikiwa tu Meno yatatumika vema Kung'ata sehemu muhimu za mwanaume.Ni silaha ambayo pengine wanaume wengi tu ndo wanaweza kuipunguza nguvu.

UONGO
Uongo ni silaha nyingine ya mwanamke kulinda uhusiano wake.Yuko tayari kusema lolote au kugeuza habari apendavyo ilimradi tu mwanaume asitoke nje ya himaya yake.
Wanajua waseme nini Kwa kasi ipi au kwa uwasilishaji upi ilimradi tu mwanaume akae sawa.Sina maana wanaume sio waongo La! Ni waongo Japo kwa ufundi,sanaa na ujuzi wa kuongopa Wanawake wanasitahili Medani.

0 maoni: