Tuesday, 10 December 2013

Mwanamke aliyedai kubakwa ahukumiwa Somalia

Mahakama nchini Somalia, imemhukumu kifungo cha nyumbani mwanamke aliyedai kubakwa pamoja na waandishi wawili wa habari waliomhoji kuhusiana na madai hayo. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19, alipewa kifungo cha nje cha miezi sita kwa kile mahakama ilisema ni kutoa taarifa zisizokweli.
Atalazimika kukaa nyumbani kwake bila kutoka nje kwa miezi sita. Mmoja wa waandishi wa habari, aliyemhoji mwanamke huyo naye alipewa kifungo cha nje cha mwaka mmoja huku mwenzake akipokea kifungo cha miezi sita.
Waandishi hao wanafanya kazi na kituo cha redio Shabelle ambacho serikali ilifunga matangazo yake mwezi Oktoba baada ya polisi kuvamia ofisi zake.

Kwa hisani ya BBC Swahili

Related Posts:

  • Full Aibu NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushi… Read More
  • Mambo ya Chuma ulete yamtokea MREMBO puani.... MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la  Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba. Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fed… Read More
  • Mke wa mtu sumu NI kweli mke wa mtu sumu! Lakini hata mume wa mtu naye sumu! Katika Gazeti la Uwazi ambalo ni ndugu damu mmoja na hili, toleo la 786, Aprili 16-22, 2013 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari kubwa; MHESHIMIWA AUMBUKA! Ka… Read More
  • Shilole aimbishwa na msanii wa Koffi Olomide? Mmmmmmh Mwisho wake sijui ilikuwaje? … Read More
  • Fulll aibu....Mfanyabiashara abambwa laivu gesti na mwanafunzi Mfanyabiashara ‘alwatani’ Bongo, mkazi wa jijini Dar, Allain Tajiri amekumbwa na skendo nzito baada ya kufumaniwa na mwanafunzi wa sekondari wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16. Tukio hilo la kusikitisha lilit… Read More

0 maoni: