Friday, 29 November 2013

Rice agundulika kuwa na saratani

Mchezaji wa zamani wa timu ya Ireland kaskazini na mlinzi wa zamani wa Arsenal Pat Rice amefikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani. Rice mwenye umri wa miaka 64 aliichezea mara 528 timu ya washika Bunduki wa London pia aliwahi kuwa Kocha msaidizi akimsaidia Arsene Wenger kwa kipindi cha miaka 16 kabla ya kustaafu mwaka 2012.
Taarifa ya klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Pat yu hospitali akipata matibabu na kumtumia salamu za pole na kumtakia heri apone haraka.

Rice aliichezea Gunners kwa kipindi cha zaidi ya misimu 14 baada ya kujiunga na timu ya vijana, ambapo timu yake ilichukua ubingwa wa Kombe la Ligi na FA mara mbili ,mwaka 1971, pia alikuwa nahodha wa Timu hiyo ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye michuano ya FA mwaka 1979.

Wenger amesifu jitihada na kazi ya Rice ambaye alikua akifanya nae kazi mpaka alipostaafu mwaka 2012.
Chanzo - BBC Swahili

Related Posts:

  • Madawa ya Kulevya yamfilisi AISHA MADINDA WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetik… Read More
  • Kaseja: sijasaini Lupopo, bado naipenda Simba KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja amesema hajasaini mkataba wa kuichezea FC Lupopo ya DR Congo ila wapo kwenye hatua nzuri ya mazungumzo lakini akasisitiza kuwa bado ana mapenzi na klabu yake ya zamani ya Simba. Ka… Read More
  • Biggest Beauty No-No's Christina hit the great trifecta of beauty fails with this one: over bronzed, invisible brows and sparse spider lashes. …to over powdering. Blend, blend, blend! Keep your lipstick from bleeding with an outer liner i… Read More
  • Malinzi achukua fomu ya urais TFF ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hi… Read More
  • Kaseja akumbwa na balaa lingine! Rais Lupopo amuita paspoti yake yaibwa KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii.&nb… Read More

0 maoni: