Friday, 29 November 2013

Jeuri ya fedha: Mke anunua TALAKA kwa milioni 4

Maharusi katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa bibi harusi (kushoto) na wazazi wa bwana harusi (kulia).

UNAWEZA kusema ni jeuri ya fedha baada ya  mwanamke, Rukia Apach kukubali kulipa shilingi milioni 4 ili apewe talaka na mumewe, Mohamed Kismati baada ya  kuzuiwa kufanya kazi na mkwewe, Ijumaa linakunyetishia. Ndoa hiyo ilifungwa miaka miwili iliyopita na kufuatiwa na sherehe ya kifahari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar mwaka juzi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wameachana kwa madai kwamba baba mkwe wa Rukia kukataa mkwewe huyo afanye kazi zaidi ya kuwa mama wa nyumbani.
Akizungumza na Ijumaa, Rukia alisema kwamba mumewe alimuahidi kumwendeleza kielimu wakati alipokuwa akisoma kidato cha sita pindi akimuoa.
“Awali mume wangu aliniahidi kuniendelea kimasomo, lakini baada ya kuolewa nikakataliwa hata kufanya kazi, amri ambayo ilitolewa na baba mkwe wangu ambaye ni mfanyabiashara,” alisema Rukia.
Mwanamke huyo alidai kwamba familia ya mumewe ilishikilia msimamo huo hadi ndoa yao ilipovunjika hivi karibuni.

Kama vile haitoshi, Rukia amedai kuwa alilazimika kulipa baadhi ya vitu na kutoa kiasi cha shilingi milioni 4 ili aweze kupewa talaka yake.
Rukia alidai kwamba chanzo cha yote kilianza baada ya baba mkwe wake kwenda Dubai kuangalia biashara zake, naye kuutumia mwanya huo kumuomba ruhusa mumewe ili akafanye kazi na kukubaliana ndipo alipoanza kazi Mlimani City, jijini Dar.
Hata hivyo, baba mkwe aliporeja akakipinga kitendo hicho na kumwambia mwanaye kwamba kumruhusu mkewe kufanya kazi ni sawa na kumtoa sadaka kwa wanaume wengine.
“Niliomba ruhusa ya siku tatu kazini ili nipate muda wa kuzungumza hilo na mume wangu lakini ilishindikana, nikaamua kurudi kazini,” aliendelea kusema Rukia.
Mwanamke huyo alisema kwamba baada ya kurudi kazini, familia ya mumewe ilimnunia na kumtaka kuondoka huku wakimzuia kuingia chumbani kwake.
“Waliniambia mizigo yangu wataniletea, nikaondoka na kurudi kwetu,”alisema Rukia kwa majonzi.

Pamoja na familia hizo kukutana na kulizungumzia jambo hilo, lakini mwafaka ulishindika ndipo upande wa mumewe ulipodai kulipwa shilingi milioni 7 kama gharama za mahari yao ili watoe talaka.
“Sikuolewa kwa pesa hizo, tukalifikisha suala hilo Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania) na kukubaliana kuwalipa shilingi milioni 4 hivyo ikawa kama nimeinunua talaka yangu,” alisema Rukia.
Mume wa Rukia, Mohamed alikiri kutokea kwa jambo hilo na kusisitiza kuwa alimuoa mwanamke huyo na hivyo alipaswa kufuata matakwa yake, vinginevyo ndiyo sababu kubwa ya kumuacha.
Familia hizo zilikutana Bakwata Jumatatu iliyopita na Rukia akakabidhiwa vitu vyake alivyoviacha kwa mumewe pamoja na pete ya ndoa.
Tafrani ilizuka baada ya mama mkwe kudai arejeshewe pete aliyovikwa mke huyo siku ya harusi, akimwakilisha mwanaye ambaye hakuhudhuria kikao hicho.
Shehe wa Bakatwa (jina halikupatikana) aliwataka kukubaliana na aya ya 20 katika Surat Nisai ambayo inakataza kumdai mali yoyote ile uliyomzawadia mkeo.
“Mlioana kwa hisani na muachane kwa hisani isitoshe unapomuacha umeshamtumia si vyema kumdai mali uliyotoa,” alisema shehe huyo.

Picha zaidi fungua hapa - GPL

Related Posts:

  • Apofuliwa macho kwa kutembea na mke wa Polisi AMA kweli haki hakuna. Katika hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar, (28) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya kuchomwa sindano inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia ku… Read More
  • Baby Madaha afunguka .....watu watachonga mengi lakini abadani sitosikiliza maneno yao STAA wa filamu Bongo anayetamba na ngoma yake ya Summer Holiday amesema kuwa kutokana na mahaba mazito anayopatiwa na mwandani wake Joe Kariuki ambaye ni Meneja wake hafikirii kumuacha kamwe. Akipiga stori na paparazi… Read More
  • Fumanizi la LULU, YOUNG DEE utata MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa n… Read More
  • Mwalimu afa kimiujiza Mwalimu Gloria Tarimo ‘Ticha Gloria’ (29) aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Mbezi High School ya jijini Dar, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakidai kifo chake ni… Read More
  • Penzi la AFANDE SELE na MAMA TUNDA kwisha? Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Shiengo ‘Mama Tunda’, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani. KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi ‘Af… Read More

0 maoni: