Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya Toyota Vitz yenye no za usajili - T929 CCX (pichani juu) leo mchana katika eneo la Sayansi-Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo majambazi hayo yalifanikiwa kumjeruhi dereva wa gari hilo sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa na fedha kiasi cha fedha shilingi milioni 40 za kitanzania na kutokomea nazo.
Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
0 maoni:
Post a Comment