Thursday, 23 May 2013

Sheha wa Tomondo omamwagiwa Tindikali Zanzibar

Jana usiku mtu asiyejulikana alimvamia Sheha wa Tomondo Mohammed Omary Said (pichani) na kumwagia Tindikali sehemu za uso na kifua na kumsababishia  majeraha na maumivu makali, tukio hilo lilitokea jana usiku wakati Sheha huyo  alipotoka  nje ya nyumba yake  kwenda kuchota maji.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Mukhadam Khamis,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pia amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole. Kwa sasa Sheha huyo anaendelea na matibabu  katika hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja

0 maoni: