Monday, 11 February 2013

Gari la Marehemu KANUMBA akabidhiwa Dr. CHENI?


IMEBAINIKA kuwa lile gari la aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, aina ya Toyota Lexus limekabidhiwa kwa mwigizaji, Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’. Kwa mujibu wa chanzo makini, mama wa marehemu, Flora Mtegoa alifikia uamuzi wa kumkabidhi Dk. Cheni gari hilo baada ya kushindwa kuligharamia mafuta. “Lilikuwa linakaa muda mrefu pale nyumbani kwao Kimara-Temboni (Dar) bila kutumika ndipo bi mkubwa akaona bora amkabidhi Dk. Cheni ili angalau aliendesheendeshe lisiharibike,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.
DK. CHENI LIVE TABATA
Wakati mapaparazi wakianza kazi ya kuchimba data zaidi juu ya gari hilo, Februari 9, walimnasa Dk. Cheni akiingia na gari hilo kwenye arobaini ya marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ iliyofanyika nyumbani kwake Tabata-Bima, jijini Dar.

LIMEPIGWA BEI? 

Kwa mujibu wa Dk. Cheni kwa sasa gari hilo lipo mikononi mwake akilitumia kwa safari za hapa na pale ili kulifanya lisiharibike vifaa kwa kukaa muda mrefu bila kutumika. “Wamenipa nilitumie kwa muda kwani lingeendelea kukaa pale basi lingeendelea kufa baadhi ya vifaa, wala halijapigwa bei,” alisema Dk. Cheni.

Katika hatua nyingine, kauli ya mama Kanumba kuhusiana na gari hilo ilitofautiana na ya mdogo wa marehemu, Seth Bosco ambapo mama huyo alisema gari hilo halijatoka nyumbani huku mdogo mtu huyo akisema limetoka. “Mbona gari lipo hapa nyumbani halijatoka, kwanza limeisha bima na matairi hayana upepo sasa litatokaje?” alihoji mama Kanumba. Seth alipoulizwa kuhusiana na uwepo wa gari hilo nyumbani, alitiririka: “Gari limetoka kwa muda hata hivyo ni bovu na linahitaji marekebisho kidogo.”


Kwa hisani ya - GLP

0 maoni: