Monday, 11 February 2013

Diamond afunguka kuhusu PENNY... adai yeye ndio kila kitu... Waridi la moyo wangu

Penny
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na minong'ono kibao kitaa kuhusu  mahusiano ya kimapenzi kati ya  Diamond Platnumz na mtangazaji wa DTV VJ Penny , habari hizo zimesambaa na kushika hatamu kwenye baadhi ya mitandao ya jamii  na hata baadhi zikionyesha wawili hao wakiwa kitandani pamoja ndani ya pozi la kimahaba....

katika kutaka mzizi wa majungu na kumaliza kufunga midomo ya wadaku wa mjini  juzi Diamond aliamua kupost picha ya Penny (hiyo juu) kwenye mtandao wa Instagram na kuandika: #MaBabyMama #De’MumOfMyBlood #MamaYounDiamond #YounPlatnumz #YoungPrezident…..



Sasa hapo utata ulizidi baada ya PENNY kuonekana kwenye tamasha la Diamond huko Kigamboni akiwa sambamba na Mama Mkwe na Marafiki wa Diamond (kama zinavyoonekana hapo chini)

 Mama yake Diamond (katikati), Penny kulia na rafiki wa Diamond

Diamond (katikati) akiwa na Penny (wa tatu kutoka kushoto) na washkaji

Sasa hapo ndugu msomaji akili mukichwa....... Hope PENNY ataweza kutuliza Diamond  manake hatutaki kusikia mambo kama ya We..... na Jo....... KIla la heri

0 maoni: