Mwenzangu sikufundishi tabia mbaya ila ukikalia kufuatilia mambo uliyofundishwa kwenye kitchen party na kwa mashoga utajikuta unakufa na kuzikwa mzimaaaa hapa mjini! hizi issue za simu zinaboa kweli na haya mambo ya kusema eti simu ya mumeo au mpenzi wako usiguse ili uepushe matatizo mimi sikubaliani nalo! utajikuta unakufa kwa kuletewa mke mwenza ndani ya nyumba..... ziba ufa mama usije ukajenga ukuta... Mijanaume mingine hata ukiionyesha mapenzi ya kijini umalaya haiachi ng'o kutwa kucha kazi ya kufungua zipu hata uwe mzuri kama malaika kazi bure! kinachonikera sana ni pale unakuta hilo janaume linaenda nyumba ndogo au kwenye makumbi ya starehe akiulizwa umeoa utasikia no dear bado nipo nipo sana sijapata nimpendaye labda nitakuoa wewe .... Nyooo hapo pete kavua na kwenye simu unaweza kukuta kakusave jina la ajabu ambalo hujawahi hata kuliwazia Kama mimi nakudanganya fanya hivi halafu utakuja mwenyewe kunipa jibu.... Chukua simu yake, kisha kwa kutumia simu yako mpigie na uangalie jina litakalotokeza kwenye screen ya simu yake, sasa hapo ndio utajua nafasi yako kwake ...
Ukikuta, darling, sweet, wife , honey, la azizi, asali wa moyo , na maneno mengine mazuri kama hayo hongera sana,jipongeze ujue umemfikisha, na hapo shosti ndio ujishikilie haswa manake anaweza akakutana na masweet wengine ukaachwa unatoa macho kama fundi saa.
Ukikuta, darling, sweet, wife , honey, la azizi, asali wa moyo , na maneno mengine mazuri kama hayo hongera sana,jipongeze ujue umemfikisha, na hapo shosti ndio ujishikilie haswa manake anaweza akakutana na masweet wengine ukaachwa unatoa macho kama fundi saa.
Pia usishangae ukikuta umeseviwa kwa jina la ajabu kama zoba, mwizi, jambazi, mvivu, fisi maji, malaya, fuska, champombe , mkorofi, cha wivu, buzi, mchawi, kidumu, bondia au labda hujaseviwa kabisaaaa ukipiga simu inatoa no tu hapo dada lazima nikupe pole ila kaza moyo ,usijali dunia ndivyo ilivyo mpenzi wako ndiyo nafasi aliokupa ndani ya moyo wake na wala usikate tamaa ukakonda kwa mawazo kwani ulizaliwa nae huyo? hukuzaliwa nae nyosha mikono juu muombe mungu nawe upate wa kukuita sweetheart.
Angalizo
Zoezi hili linahitaji uvumilivu na ujasiri wa hali ya juu, ukimaliza hii kazi rudisha simu yake haraka ulipoitoa, kaa kimya na ufanye siri ili usijulikane manake unaweza shangaa ukaanzisha zogo kutokana na jina ulilosaviwa uchune wala usionyeshe dalili yoyote, zoezi hili ni zuri kama ukiwa jasiri kwa sababu litakusaidia kujua nafasi yako kwa mume wako au mpenzi wako , kama umeseviwa kwa jina baya utajirekebisha hadi afute hilo jina na kukusevu kwa jina zuri, kama jina zuri basi utazidiha mambo fulani ili azidi kuchanganyikiwa hadi aukite malaika wangu aaaaaa..
0 maoni:
Post a Comment