Friday, 29 August 2014

Je unamjua Askofu bilionea Tanzania? Angalia baadhi ya picha za mikutano yake hapa.....

 ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe.
 Hapa akionekana katika moja ya mikutano yake alipokuwa Karatu mkoani Manyara, inasemakana kuwa Askofu  Geordavie  hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, na mara zote huwa  na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.

 Mbali  na kumiliki  chopa ambayo ameinunua , askofu huyo huambatana na msururu wa magari yenye thamani kubwa kwenye mikutano yake kiasi cha kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.

 Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.


Baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.


Waumini wengi wamelalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi huyo kutokana na ulinzi mkali anaopewa, Imefahamika kuwa  utajiri wake hakuna mfano na  nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” 

Related Posts:

  • Mwinjilisti aua mke, ajinyoga MKAZI wa Kijiji cha Gama, wilayani Bagamoyo, Elikia Daniel (35), ambaye pia ni Mwinjilisti wa Kanisa la Anglikan katika kijiji hicho, amekutwa amejinyonga baada ya kufanya ukatili wa kumuua mke wake, kwa kumkata panga kichwa… Read More
  • Hatimaje Mama LULU na Mama KANUMBA waenda BUKOBA kula kiapo cha Undugu Kutoka kushoto: Flora Mtegoa, Lulu na Lucresia Karugila katika pozi. ULE udugu wa ukubwani kati ya wazazi wa mastaa wa filamu Bongo, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na  Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ umezidi kukua kufua… Read More
  • Justin Bieber akamatwa na polisi Mwanamuziki mashuhuri duniani Justin Bieber,amekamatwa na polisi nchini Marekani kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi. Polisi katika mji wa Miami Beach, wamesema kuwa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 19 pia ali… Read More
  • Abakwa kwa amri ya wazee wa kijiji India Mshukiwa wa kitendo cha ubakaji Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi. Inadaiwa wanaume, hao walim… Read More
  • Rihanna full bata Kwa habari kamili fungua hapa - Rihanna full bata … Read More

0 maoni: