Tuesday, 18 March 2014

Villas- Boas kujiunga na St.Petersberg

Aliyekua Kocha wa Tottenham na Chelsea, Andre Villas-Boas ameridhia kuingia mkataba wa miaka miwili na klabu ya Zenit St Petersburg, taarifa za klabu hiyo ya Urusi zimeeleza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36, aliyetimuliwa na Spurs mwezi Desemba atachukua nafasi ya Luciano Spalletti. Villas-Boas atatangazwa rasmi kuwa Kocha mkuu wa Timu hiyo tarehe 20 mwezi Machi.
Kibarua cha Spalletti kiliota nyasi baada ya Spurs kupoteza mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora ambapo ilipigwa mabao 4-2 na Borussia Dortmund.
Villas-Boas alikuwa sehemu ya kikosi cha uongozi cha Jose Mourinho kabla ya kujiunga na Academica na Porto za nchini kwake Portugal.
Aliwezesha ushindi wa kombe la ligi, ligi ya Europa katika msimu wake wa kwanza akiwa na Porto kabla ya kujiunga na Chelsie mwaka 2011, lakini alitemwa na timu hiyo mwezi March mwaka 2012 baada ya kushindwa kuifikisha timu hiyo kwenye viwango bora.

Kwa hisani ya BBC Swahili

Related Posts:

  • Malinzi rais mpya TFF JAMAL Malinzi, jana alitangazwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kupata kura nyingi dhidi ya mpinzani wake, Athumani Nyamlani katika uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye Ukumbi wa Water Front jijin… Read More
  • Kocha Fiorentina kutua Azam Stewart Hall asema kilichomuondoa ALIYEKUA Kocha mshauri wa klabu za Fiorentina na Atlanta za Italia, Fabio Lopez anatarajia kuifundisha timu ya Azam FC ambayo kwa sasa haina kocha baada ya aliyekuwa anaifundisha Mui… Read More
  • Amigolas: Nimefanya kazi Twanga miaka 18 bila mkataba Mwanamuziki  mkongwe Hamis Kayumbu maarufu kama Amigolas,  aliyeitumikia  Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), amesema kuwa licha ya kudumu na bendi hiyo kwa miaka 18 hakuwahi kuwa na mkataba. Amigolas a… Read More
  • WAMBURA ateuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu TFF Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu. Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah… Read More
  • Juma Kaseja atua Ndanda FC? KIPA namba moja wa Taifa Stars, Juma Kaseja dili lake la kwenda kuichezea FC Lupopo ya DR Congo halieleweki na kusisitiza kuwa ameamua kujiunga na timu ya Ndanda FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa ajili ya mazoezi i… Read More

0 maoni: