Habarini marafiki zangu
Dalili:
1. Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa sio kwamba anataka muda huo awe na wewe.
2. Anakuwa na tabia za kukuudhi na kukutawala, ataangalia sana kutoka na kuingia kwako, nyendo zako na hata matumizi yako ya fedha, na kama ukimuuliza kwanini anafanya hivyo
atajiteteta kuwa anakusaidia kufanya maamuzi sahihi.
3. Taratibu anakutenga na wote waliokaribu na wewe, pia anajaribu kukutenga na wale wanaoonekana kuwa msaada kwako kama vile wale unaowasiliana nao kwa simu, wafanyakazi wenzako na hata ndugu zako wa karibu.
4. Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayoyapata yeye. Mfano anapokosa kazi, anaposhindwa shuleni, anapokosa pesa nk. Kila kitu ni kosa la mtumwingine na sio yeye.
5. Hukasirishwa na kuudhiwa na vitu vidogo vidogo na vya kawaida katika maisha ya kila siku,
mfano akiambiwa afanye kazi zaidi ya muda wa ofisi, akiombwa amwangalie mtoto, anapopingwa katika kitu kidogo nk.
6. Anakuwa na tabia za kikatili kwa wanyama wafugwao “pets” na hata kwa watoto. Haumizwi pale anapoona maumivu au kuteseka kwa kiumbe kingine. Anaweza kujiona anacheza au anatania bila kujua anamuumiza mtoto au mnyama.
7. Ni wenyetabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatojali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.
8. Ni wenye maneno makali yakuumiza na ya kushusha hadhi, huweza kukuamsha usingizini ili akutukane au kukugombeza. Akianza malumbano hakupi upenyo wa kwenda kulala, anaweza kulalama usiku mzima.
9. Sio watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu anafuraha na kuonyesha mapenzi, mara ghafla kakasirika na kutaka kuadhibu mtu.
10. Anaweza akawa na historia ya tabia za kikorofi na kigomvi, labda amewahi kuwa na matukio ya kuwapiga marafiki zake, akijitetea kuwa alipitiwa tu na hasira
0 maoni:
Post a Comment