Monday, 3 February 2014

Bongo vituko daily!!!!!! WEMA: NIKIFA NIAGWE UWANJA WA TAIFA

Kazi ipo! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda limemtegea sikio. Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo pande hizo.

Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo viwanja hivyo havitatosha.
“Mimi nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • Majonzi SAKATA la kijana Bonny Fabian Kavishe kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi baba yake, mzee Livingstone Kavishe akiamini ni mwizi sasa ni simulizi ya machozi kufuatia kusomwa kwa waraka mzito ulioandikwa na mtuhumiwa huyo amba… Read More
  • Ukahaba waligusa BUNGE BIASHARA ya ukahaba imeligusa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani Jumanne iliyopita takribani dakika nane zilitumika kuijadili inavyoshamiri na namna ya kuitokomeza. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vij… Read More
  • Mpenzi ndani ya penzi jipya? Fungua hapa usome habari kamili -GLP … Read More
  • LADY JAYDEE Vs Clouds MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, juzi Jumatatu hatimaye yalimkuta baada ya kuibua simanzi nzito katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, alipofikishwa baada ya kufunguliwa kesi ya madai namba 29/2013 na mabos… Read More
  • Ama kweli mjini shule! Ombaomba feki anaswa live.... WAKAZI wa mjini Iringa hivi karibuni wameshuhudia kituko cha mwaka baada ya kumnasa mzee mmoja akijifanya ombaomba kwa kuigiza ulemavu asiokuwa nao. Ombaomba huyo feki alijifanya hana mkono wa kushoto na mguu wa kulia… Read More

0 maoni: