Monday, 18 November 2013

More than friends?





Baaada ya Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa kunaswa kimahaba hapo jana, leo Mwanadada Snura Mushi amfunguka na kudai kuwa Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo


Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu. Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”



Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.



Hapo awali ilidaiwa kuwa wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’. Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.



“Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.  “Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.



Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona. Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.


Habari - Bongo Movies
Picha kwa msaada wa Mtandao

..................Stay Tune........................


Related Posts:

  • Kioo cha jamii! Hii picha inaleta maana gani kwa watu wanaopenda na kukubali kazi zako?  Kuwa staa lazima ufanye hivi?  Je kuna  vyombo vinavyohusika kwa watu kama hawa?  Je mila na desturi zetu zinaangaliwa? … Read More
  • Mzee wa Blig Bling full vituko angekuwa Bongo ingekuwa so Pata uhondo wote hapa - Mzee wa Blig Bling na vituko vyake … Read More
  • Mapema jana wanamuziki   Diamond Platnumz  na Mshikaji wake Ommy dimpoz kupitia kurasa zao Twitter walifanya mazungumzo yaliyoacha maswali kibao yasiyo na majibu ...... hebu soma hapa chini … Read More
  • JOSEPH SHALUWA amchana live JACK wa CHUZ Kwako, Jacqueline Pentizel ‘Jack wa Chuz’. Pole kwa changamoto ulizokutana nazo juzi hotelini wakati ukiwa na mteja aliyetaka kuspendi na wewe kwa dola 500. Ni ajali kazini, usiwaze sana.  Tatizo nini ujue s… Read More
  • Sandra akanusha kupigwa talaka.. Mwigizaji wa kike  wa Bongo Movie almaarufu kwa jina la Sandra ambaye kwa siku za hivi karibuni tuliwahi kurusha habari za kupigwa kwake talaka na mumuwe amekanusha habari hizo kupitia kipindi cha HOt MIX  c… Read More

0 maoni: