Mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambaye sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu Sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana.
Huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu mwanamke kutumia kitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandao.
Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani.
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi na hwafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi.
Watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa matapeli haya ya kimtandao.
Hiki ndio kitambulisho alichotaka kutumia huyu mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi laini sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakazi mmoja wa Tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja.
Aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya Sim Banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa ali-renew na kuiba pesa.
Kwa hisani ya GPL
0 maoni:
Post a Comment