Friday, 23 August 2013

Yanga wamuongezea adhabu Mrisho Ngassa?

IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, ndiyo iliyochangia ukubwa wa adhabu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Mrisho Ngassa, Championi Ijumaa limebaini. Taarifa hiyo inakuja wakati ambao Ngassa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano pamoja na kuilipa Simba jumla ya shilingi milioni 45, sababu kubwa ikiwa ni kusaini mikataba miwili, ule wa Yanga na ule wa Simba.
Boniface Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameliambia Championi Ijumaa kuwa, adhabu ya kufungiwa michezo sita kwa Ngassa imewekwa maalum, kutokana na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kutaka mchezaji huyo apate uchungu wa makosa aliyoyafanya na siyo kutegemea kulipiwa na klabu.
Wambura alisema adhabu hiyo imetokana na kasumba ya klabu mbalimbali ambazo zimekuwa zikiamua kulipa faini wanazokatwa wachezaji wao kwa makosa mbalimbali, maamuzi ambayo yanasababisha wachezaji kurudia makosa hayo.
“Adhabu kama hii ni maalum kuweza kumfanya mchezaji aone makali ya kosa alilofanya ili asiweze kurudia wakati mwingine, kamati imebaini kuwa makosa kama haya kila wakati yanakuwa yakijirudia kwa kuwa klabu ndizo zinazosababisha hilo,” alisema Wambura na kuongeza:
“Hata huku TFF, tunaona jinsi klabu zinavyofanya, endapo mchezaji fulani anapofanya makosa na kuhukumiwa utaiona klabu ndiyo inakuja na kuilipa faini husika, maamuzi kama hayo yanasababisha mchezaji asijue makali ya makosa anayofanya, ndiyo maana adhabu hii ikawa kali zaidi.”

Kwa hisani ya Khatimu Naheka/GPL

Related Posts:

  • Jeuri ya fedha: Mke anunua TALAKA kwa milioni 4 Maharusi katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa bibi harusi (kushoto) na wazazi wa bwana harusi (kulia). UNAWEZA kusema ni jeuri ya fedha baada ya  mwanamke, Rukia Apach kukubali kulipa shilingi milion… Read More
  • Ndoa ya THEA and MIKE yavunjika? SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’ kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisem… Read More
  • Dunia ina mambo !......Kijana wa miaka 32 answa na kibibi kizee cha miaka 80 Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa. Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi hu… Read More
  • Apofuliwa macho kwa kutembea na mke wa Polisi AMA kweli haki hakuna. Katika hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar, (28) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya kuchomwa sindano inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia ku… Read More
  • RAY, CHUCHU HANS laivuuuu AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘l… Read More

0 maoni: