Saturday, 3 August 2013

Redio ya SHAROimenifanya mauzauza

MSANII wa Kundi la Green Masage, linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya TBC, Daniel Mmasi ‘Face Brown’ amefunguka kuwa redio ya marehemu Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ aliyoinunua, imemletea mauzauza Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Daniel alisema alinunua redio hiyo ya ‘sabuufa’ kutoka kwa kijana aliyejulikana kwa jina la Suleiman (dalali wa mali za Sharo), lakini  anapoizima usiku, huwa inajiwasha yenyewe.
“Niliichomoa kwenye umeme wakati wa kulala, ghafla usiku nikasikia inazungumza wakati sikuichomeka umeme, kuna siku nilikuwa narudi nyumbani kwa dirishani nikasikia inazungumza wakati asubuhi niliizima,” alisema Daniel ambaye ameamua kuirudisha redio hiyo kwa dalali bila kurejeshewa malipo yake.

Kwa hisani ya  Imelda Mtema/GPL

0 maoni: