Friday 31 May 2013

FA & JAYDEE waahirishwa show zao kutokana na kifo cha Magwea...

KUTOKANA na habari za kufariki kwa Albert Mangwair ‘Ngwea’, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ ametangaza kuahirisha shoo yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike leo (Ijumaa). 

MwanaFA amesema ameamua kufanya hivyo ili kupisha maombolezo ya msanii huyo maarufu, baada ya hapo atatangaza siku nyingine ya kufanya shoo hiyo.

“Nawaomba radhi mashabiki wangu hasa waliokata tiketi, wawe na subira kwani hili limetokea na ni letu sote. Tarehe ya shoo tutaitangaza baada ya mwili wa marehemu kupumzishwa kwenye nyumba ya milele,” alisema msanii huyo.

Aidha, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ naye ameahirisha shoo yake ya kutimiza miaka 13 tangu alipoanza gemu la muziki ambayo ingeenda sambamba na uzinduzi wa albamu yake iitwayo Nothing But the Truth iliyokuwa ifanyike leo.

Kwa hisani ya GLP

0 maoni: