Tuesday 16 April 2013

Kuna ukweli wowote kwenye hili?

Ni muda sasa nimekuwa nikiangalia au kufuatilia hii kesi ya Lwakatare kupitia TV hususani wakati wa taarifa ya habari. Lakini nimekuwa sielewi ishara anayoonesha bwana Ludovicky ya vidole viwili alama ambayo inatumika kama utambulisho kwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA.

Shida ninayoipata ni pale wafuasi wa CHADEMA na of course viongozi kumshutumu kuwa ametumika kuandaa ile video, sasa kwa yeye kusaliimiana na wafuasi kwa kutumia hiyo ishara huku akituhumiwa kuwa moja ya walioshiriki kukihujumu chama sasa ni kwamba ANAJIPENDEKEZA au AMEWASALITI hao waliomtumia?

Mdau J

0 maoni: