Tuesday 16 April 2013

Je unajua dalili za Mwanaume mwenye nyumba ndogo? soma hapa ...


1. Utaambiwa safari za kikazi za kila mara
2. Mikutano kazini inayofanyika hadi baada ya muda rasmi wa kazi kila mara
3. Wa mwisho kulala na wa kwanza kuamka asubuhi
4. Akilala, hulalia ubavu mmoja usiku mzima
5. Anachoshwa na “shughuli za kazini”, hapendi mai waifu wake amsogelee wakati wa kulala
6. Utanashati utaongezeka maradufu kuliko kawaida yake
7. Mawasiliano ya simu na mai waifu wake hupungua ghafla au kukatika kabisaa
8. Kubana matumizi nyumbani ( Nyama kuliwa mara 1kwa wiki)
9. Nyumbani dagaa ndiyo kitoweo cha kawaida
10. Friji itaanza kuwa ya maji ya kunywa badala ya soda na vibia kidogo kwa ajili ya wageni
11. Wali utaanza kuliwa siku za sikukuu tu
12. Matunda atakula yule tu atakayekuwa mgonjwa na amelazwa hospital kwa maagizo ya daktari
13. Mkali sana nyumbani kwa familia kuhusu matumiziya maji.
14. Familia kutakiwa kutumia pasi na jiko la mkaa ili kupunguza matumizi ya umeme.
15. Mkali kama simba arudipo kutoka “kazini” hana mazungumzo na familia yake.
16. Hata akienda chooni haachani na simu yake
17. Huonekana mwenye mawazo sana anapokuwa nyumbani kwake

Ukiona hivi mwanamke mwenzangu tafuta njia ya kumnasua ........

0 maoni: