Friday, 1 February 2013

Nimefanikisha kumtoa LULU sasa naamia kwa Kajala

STAA aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ anapata dhamana, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kwa Lulu sasa anahamia kwa msanii mwingine, Kajala Masanja. Akizungumza nje ya Mahakama Kuu jijini Dar baada ya Lulu kuachiwa, Dk. Cheni alisema kwa sasa anaanza mchakato wa kumsaidia Kajala mpaka ajue hatima ya kesi  inayomkabili.

“Unajua Lulu siyo mtu wa kwanza kumsaidia na mama yake ndiye aliniomba, nilishawasaidia wengi. 

Hata Cloud alipofungwa nilifuatilia mimi na Dude mpaka mwisho, hatukukata tamaa na kwa Kajala nitafanya hivyo kwa sababu ni mwenzetu jamani, naamini Mungu anaweza sana na atafanikisha kila kitu,” alisema Dk. Cheni.

Kajala anasota Segerea akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na serikali kutokana na mumewe kutakatisha fedha haramu.

Related Posts:

  • Demu Mzungu wa Magwea awatoa watu machozi MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alik… Read More
  • Mahojiano kati ya Millard na M To The P Leo Millard Ayo ameingia kwenye wodi aliyolazwa rafiki  wa marehemu Gwair M 2 the P na kufanikiwa kufanya mahojiano nae. M 2 the P alikiri kupata nafuu ila alilalamika kuwa kichwa na kifua bado vinamsumbua, katika m… Read More
  • Kifo cha Magwea chamchanganya TID JUMANNE wiki iliyopita haikuwa poa hata kidogo kwa Watanzania wengi wapenda burudani. Alifariki dunia Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwea’, rapa wa Kibongo. Mbaya zaidi ishu hiyo ilitokea huko Johannesburg, Afrika Kusini au Sauz… Read More
  • Who is she? Full news and more photos click here - Lil Kim … Read More
  • Mimba yamtesa PENNY TUMEINYAKA kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV, Ijumaa Wikienda linashuka nayo.… Read More

0 maoni: