‘Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni’. Usemi huu umethibitika hivi karibuni baada ya mlokole mmoja, Ruth Mwakalinga, mkazi wa Matejo, Arusha kumnywesha damu ya hedhi mwanaye, Easter Deodat. Akizungumza na Risasi Jumamosi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Easter alisema kuwa, wazazi wake walimfanyia kitendo hicho kwa tamaa ya kumiliki mali. “Baba na mama waliamua kunifanyia hivyo kwa lengo la kunipumbaza akili ili niwe ndondocha na wao wawe matajiri,” alisema.
Easter alisema kuwa, siku ya tukio alitoka ndani kwa lengo la kutupa uchafu baada ya kupata siku zake (hedhi) lakini alistaajabu mama yake huyo wa kambo alipomfuata na kumzuia ili arudi ndani.
“Nilipoingia ndani aliniuliza nimebeba nini mkononi, nikamwambia sina kitu, cha kushangaza aliniambia niuchukue uchafu huo kisha niikamulie damu hiyo kwenye kikombe alichonipa,” alisema Easter huku machozi yakimtoka.
Msichana huyo aliendelea kueleza kuwa, baada ya kuikamulia damu kwenye kikombe, aliambiwa aendelee na kazi zake. Kesho yake asubuhi aliitwa chumbani kwa mama yake na kulazimishwa kuinywa damu hiyo.
Baada ya kuinywa alipoteza fahamu na alipozinduka alijiona akiwa tofauti na siku nyingine. Tangu siku hiyo alikuwa anatokwa na damu kila sehemu yenye uwazi.
Habari zaidi endelea kufuatilia gazeti la RISASI
0 maoni:
Post a Comment