Thursday, 27 June 2013

Tumsaidie Mtoto Hamisi tumuokoe kwenye mateso!

Tafadhalini msaada wadau! Mtoto Hamis Hashim Bakari, mwenye umri wa miaka 13, anapata mateso makubwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kujaa maji kutokana na kugundulika kuwa na mifupa laini tangu mwaka 2008.  Mtoto Hamis anaishi na wazazi wake Yombo Dovya, jijini Dar. Tatizo lake lilianza alipovunjika mguu wa kushoto ambao ulijaa maji na kuvimba.

Katika harakati za kupata matibabu, Hamis alitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kugundulika tatizo na akawa ameshindwa kutembea huu mwaka wa tano sasa.

Muda wote Hamis anatambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku safari ndefu akizifanya kwa msaada wa baiskeli aliyopewa na Shule ya Msingi ya Yombo Dovya.

Kufuatia mateso anayopata kila kukicha, Mtoto Hamis anaomba wasamaria wema kutoka sehemu mbalimbali wamsaidie ili kufanikisha matibabu na huduma nyingine.

Mwenye msaada wowote wa hali na mali kwa Mtoto Hamis, tuma au wasiliana na simu namba 0784211085 au0714452275.


Kwa hisani ya Chande Abdallah na Denis Mtima/GPL
Picha zaidi fungua hapa - "Mtoto Hamis Hashim Bakari."

Related Posts:

  • BARNABA awaliza watu kwenye mazishi ya mama yake, aishiwa nguvu na kupoteza fahamu ........ Barnaba akiaga mwili wa mama yake Haikuwa rahisi kwa Barnaba kumuaga kipenzi chake Baada ya  kuweka mchanga kaburini Barnaba aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa Hapa akip… Read More
  • 15 famous people who mysteriously disappeared Though many of them are presumed dead, exactly what happened to these high-profile personalities still remains unknown. The Lost Roanoke Colony. The Dyatlov Pass Incident. The death of Natalie Wood. The Black Dahlia. … Read More
  • Mtaa wa ngono wafumuliwa.... NI hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani, Operesheni Fichua M… Read More
  • Mimba ya Penny yatoka? TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa. Kwa mujibu wa chanzo makini kili… Read More
  • 5 Signs You Are Not as Smart as You Think It’s a concept that can be difficult to come to terms with, but like it or not our intellect (or our perceived intellect) can often work against us in life. The indications are all there once you have the eyes to see them.… Read More

0 maoni: