HAIWEZI kuwa aibu mpaka siri ifichuke, kwa wake za watu 13 walionaswa wakijiuiza, kwao imekuwa zaidi ya kuumbuka, wametia fedheha ndani ya familia zao. Wake hao za watu, walinaswa usiku wa Jumanne iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Afrika Sana mpaka Mori, Sinza, Dar es Salaam, wakati jeshi la polisi lilipofanya msako maalum wa kushtukiza.Pamoja na wake hao za watu, vilevile wanafunzi 18 wa vyuo mbalimbali nchini, mahausigeli saba na mabaamedi watano, arobaini yao ilifika siku hiyo, walipokamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Mabatini kabla ya kupandishwa kizimbani, Mahakama ya Jiji siku iliyofuata.
Katika msako huo, zaidi ya makahaba 60 walikamatwa na katika mahojiano na polisi, ikabainika kuwapo kwa wake hao za watu, wanafunzi, wahudumu wa baa na wafanyakazi wa ndani.
WAKE ZA WATU
Jeshi la polisi likichukua maelezo ya mmoja baada ya mwingine, askari mmoja alimfikia mwanamke aliyefahamika kwa jina la Suzan Moses ambaye katikati ya mahojiano, alijieleza kwamba ni mke wa mtu.
Suzan ambaye baadaye ilibainika kwamba hujulikana pia kwa jina la Mamaa Suzy, alijieleza kuwa anaishi na mume wake (jina tunalo), Tandale, Dar es Salaam na wana watoto wawili. Askari aliyekuwa anamhoji Suzan, aliuliza: “Mke wa mtu kweli na watoto wawili unajiuza, huoni kama ni hatari?”
Suzan: “Hatari naijua ndiyo maana simruhusu mwanaume yeyote aniingilie bila kondomu, nipo makini juu ya hilo.”
Askari: “Mumeo anajua kama unajiuza?”
Suzan: “Hajui, japokuwa hata yeye tulikutana viwanja. Nilimdanganya mimi ni mhudumu wa Corner Bar, akaniachisha kazi lakini baada ya kuona hanitimizii mahitaji muhimu, nikamwambia narudi kazini, kwa hiyo mpaka leo anajua nahudumia baa.”
Baada ya wote kuhojiwa, ikabainika kuwa katika wanawake hao 60 waliokamatwa, mbali na Suzy, walikuwepo wengine 12 ambao ni wake za watu.
Mwanamke mwingine, Jessica Mashaka alidai kuwa aliamua kujiuza baada ya kubaini kwamba mume wake analelewa na mwanamke mmoja tajiri jijini Dar es Salaam.
“Anachokifanya mume wangu ni sawa na mtu anayejiuza. Akipewa fedha na mwanamke wake ananinyanyasa ndani ya nyumba, nikaona na mimi nijiuze nipate fedha zangu mwenyewe ili aache kuninyanyasa.”
Hata hivyo, Leila Madaha alidai yeye na mume wake walikubaliana ajiuze ili wawe wanapata fedha za kujikimu. Alisema: “Mume wangu huwa ananisisitiza kutumia kondomu kwa kila mteja, yeye hana kazi tangu alipofukuzwa bandarini miaka minne iliyopita.”
MADENTI
Wanafunzi 18 kutoka vyuo vya Dar es Salaam, Dodoma na Iringa, walijitambulisha katika mahojiano na hayo na polisi. Hata hivyo, majina ya vyuo walivyodai wanasoma, tunayahifadhi mpaka pale tutakapothibitisha kile ambacho wao wenyewe walikieleza.
Wanafunzi wa mikoani walisema kuwa hali ni mbaya kibiashara huko tangu iingie Januari ndiyo maana wamekuja Dar kujaribu kutafuta kipato. “Kule Dodoma hali si nzuri, najua hivi karibuni bunge litaanza, Dom itachangamka, biashara itakuwa nzuri lakini kwa sasa hakuna wateja na mahitaji hatuna. Binafsi nangoja nimalize chuo nipate kazi yangu, hamtaniona nikijiuza. Hizi ni shida tu,” alisema mmoja wa madenti hao.
MABAAMEDI NA MAHAUSIGELI
Katika wanawake hao, ilibainika wapo mabaamedi watano ambao walidai kuwa vipato vyao ni vidogo ndiyo maana kila baa wanazofanyia kazi zinapofungwa saa 5:00 usiku, hulazimika kuingia mitaani kuuza miili waweze kupata fedha zaidi za kuwawezesha kuishi.
Vilevile, wapo mahausigeli saba ambao maelezo yao yalikuwa sawa na yale ya mabaamedi kwamba hulipwa ujira mdogo na mabosi wao ndiyo maana hulazimika kujiuza ili kuongeza vipato.
Angalia picha zaidi hapa chini
Kwa hisani ya http://www.globalpublishers.info
0 maoni:
Post a Comment