Sunday, 20 January 2013

Mastaa wa BONGO full vituko

IMEVUJA kuwa chanzo cha bifu, migongano, mtifuano na mpasuko baina ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ni kugombea mabwana, wivu, chuki na vita ya kufunikana na kila mmoja kujiona yupo juu kisanii, IJUMAA linafunguka. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya mastaa hao huingia kwenye migogoro baada ya kuingiliana kwenye anga zao, wanaume.

WOLPER NA UWOYA

Ilifichuka kuwa kiini cha bifu la mastaa wawili vinara wa mauzo ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Irene Uwoya linalozidi kufukuta kwa kuongezeka kwa chuki na kukomaa mizizi kila kukicha ni mwanaume.


Ukiachilia mbali hivi karibuni ambapo Uwoya alidaiwa kula njama na ‘bodigadi’ wake aitwaye Mariam Ismail aliyemtwanga Wolper, huko nyuma wawili hao waliwahi kudaiwa kugombana kisa wivu wa kimapenzi wakimgombea bwana aliyekuwa mchumba wa Wolper aliyejulikana kwa jina moja la Ababuu.

Ilifahamika kuwa mbali na chuki na wivu wa kimapenzi, Uwoya na Wolper hawaivi kwa sababu kila mmoja amekuwa akidai yupo juu kimaisha zaidi ya mwenzake.

Habari za ndani zilieleza kuwa kila mmoja amekuwa akijitapa kumfunika mwenzake kisanii, jambo ambalo liliibua hisia tofauti kwa baadhi ya watu waliomnyooshea Uwoya kidole kuwa ni kweli ameshuka.

Wolper alipotakiwa kuzungumzia bifu lake na Uwoya alisema ameliacha suala lao kwa uongozi wa Bongo Movie huku Uwoya akiwa tuliii.

WEMA NA AUNT
Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson, nao wanatajwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kwamba ni kilekile, yaani kila mmoja kujiona yupo juu kuliko mwingine.

Hivi karibuni mambo yalikwenda kombo kati ya wawili hao ambapo Wema alimtuhumu Aunt kushindwa kuhudhuria pati aliyokuwa ameiandaa kwa ajili ya mastaa wenzake ya kuukaribisha mwaka 2013 bila sababu ya msingi, akisahau kuwa yeye (Wema) alikuwa naye bega kwa bega wakati wa maandalizi hadi ndoa yake aliyofunga na Sunday Demonte. 

Hata hivyo, Aunt alijaribu kuomba msamaha lakini Wema alikuwa mgumu kumsamehe kwa kusema hana hamu naye.

UWOYA NA FLORA MVUNGI
Pia uchunguzi wetu ulibaini kuwa Uwoya na Flora Mvungi hawaivi hata tone kufuatia lile sakata la matusi ya nguoni kisa kikiwa penzi la Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’.

Ilielezwa kuwa kisa cha yote ni wivu wa kimapenzi kwa H. Baba ambao uliwajengea chuki na hadi leo hawajawahi kukutana uso kwa uso ikiaminika siku wakikutana, patachimbika au kutoana roho.

FLORA NA SHILOLE
Uchunguzi huo ulibaini kuwa Flora mwenye lugha kali kwa wenzake, hivi karibuni alinogesha bifu na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ baada ya kumwambia kuwa ananuka wanaume.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Shilole, mwigizaji huyo ambaye pia ni mwanamuziki ameweka mtego wa kumnasa Flora ili amshikishe adabu.

kwa hisani ya GLP

0 maoni: