Tuesday, 15 January 2013

Man Walter Amaliza Beef Yake Na Wasanii Wote Akiwemo 20%...

Producer wa muziki maarufu nchini, Man Walter (pichani kushoto) atangaza kumaliza beef zake zote alizokuwa nazo na wasanii. Akizungumza na radio moja maarufi nchini, Man Walter alizungumza kumaliza matatizo yote aliyokuwa nayo na wasanii ikiwemo hata yale ambayo hayajulikani 
     Akizungumzia kuhusu 20%, Man Walter alisema beef yake na 20% ni moja ya matatizo ambayo yalikuwepo na sasa hayataki tena, yuko tayari kufanya kazi na msanii wowote ikiwemo 20%.



     Akiongelea beef zingine, Man Walter alisema wapo wasanii au watu ambao unaweza kuwa na matatizo nao bila kujua, mtu ana beef na wewe ya kichini chini lakini mimi nimeyamaliza yote.

Kipindi fulani nyuma, producer Man Walter aliingia kwenye beef na 20% na kushindwa kuendelea kufanya kazi na msanii huyo ambaye wamefanya kazi nyingi pamoja.


0 maoni: