Wednesday 23 January 2013

Jack Wolper full mawazo......

Hakika sasa naamini kuwa kua uyaone...... 

Kuna habari zenye chanzo cha uhakika zimezagaa mtaani eti Msanii wa filamu  za kibongo, Jackline Wolper, ambaye inadaiwa kuwa ndiye anayewafunika mademu wenzake kwa kuwa na mkwanja mrefu, hivi karibuni amekuwa akiwaza sana  suala zima la nani atamnasa ili amuhonge vitu vya kifahari kama Dallas?

Habari hii ni ya uhakika kwani anayeivujisha ni  Shosti wake mkubwa! huyo shost alijikuta akiropoka na kusema sasa hivi Jack hana wanaume anayeweza kumpa vitu ya kifahari kama ilivyokuwa anapewa na Dallas yaani siku hizi hata misheshe za kutoka hapa na pale zimepungua  yaani full kukaa home ! kama haitoshi shost huyo alizidi kufunguka na kusema“Rafiki yangu bado hajapata mtu bwana najua ungeona kelele za mjini, saivi yupo tu kama hivi hamna mpya” 

Wambeya wa mji kama kawaida wakaona isiwe tabu wakaamua kupita mlango wa nyuma na kutaka kujua hii habari  ni kweli au porojo za mji? Cha ajabu  Wolper aliruka kimanga na kugoma kuzungumzia ishu ila alidai kuwa hakuna mtu anayejua siri zake na kama kuna mtu anajua basi abaki na hizo alizonazo.....

0 maoni: