Monday 17 June 2013

Kajala awekwa mtu kati..... afunguka kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na PETIT

LEO tunatimiza ahadi yetu kwako kuwa wiki hii utamsikia staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja akijibu na kufafanua laivu maswali mliyomuuliza wiki iliyopita. SHUKA NAYO…
Kajala akimlisha keki Petit Man wakati wa sherehe yake ya kukaribishwa uraiani.
UFAGIO, OMBI
Nakupenda sana Kajala naomba niwe ndugu yako wa hiyari. Rishmer, Dar, 0717087228
KAJALA: Sawa.

ALITOA RUSHWA YA NGONO?
Kajala kuna tetesi kwamba wakati unataka kuwa mwigizaji ulikataliwa lakini ulivyotoa rushwa ya ngono ukakubaliwa, je, kuna ukweli? Issa Chongono, Tanga, 0714455748
KAJALA: Si kweli.

KUHUSU MUMEWE GEREZANI
Kajala mambo vipi? Nasikia kuwa tangu utoke gerezani na kuwa huru hujawahi kwenda kumuona mumeo, kwa nini? Timothy, Dar, 0718185998
KAJALA: Kila wiki huwa nakwenda kumuona na kama nimesafiri anakwenda mdogo wangu.

POLE KWA MATATIZO
Hongera mwanangu kwa uigizaji wako na pole kwa matatizo, tulikumisi sana mashabiki wako. Msomaji, 0653767053
KAJALA: Asante, nimerudi subiri kazi mpya zinakuja nyingi sana.

YEYE NA PETIT MAN
Kajala ni kweli unatoka kimapenzi na Petit Man wakati mumeo yuko gerezani? Riziki Minde, Dar, 0716000045
KAJALA: Siyo kweli.

YEYE NA P-FUNK
Nakukubali sana dada, naomba kujua mlidumu na P-Funk kwa miaka  mingapi? Mwasiti, Dar, 0718787845
KAJALA: Miaka tisa.

APIGE KAZI
Dada Kajala mimi nakupenda wewe! Nimefurahi sana uliporudi kwenye kazi yako, pole kwa mitihani iliyokukuta, bado uwezo unao piga kazi na epuka skendo zitakuharibia. Sauda, Moro, 0767466809
KAJALA: Asante kwa ushauri, nitaufanyia kazi.


SHULE VIPI?

Kajala napenda sana filamu zako nzuri zenye ujumbe wa kuelimisha jamii, je, vipi kuhusu kiwango chako cha elimu? Salim Liundi, Dar, 0658110395
KAJALA: Nina elimu ya kidato cha nne pia nilisomea IT lakini sikuifanyia kazi.

HUWA ANAMTEMBELEA MUMEWE?
Dada Kajala nakupenda sana hasa muonekano wako, vipi mumeo huwa unaenda kumuona gerezani au ndoa tena hakuna? Tumaini, Dar, 0712312932
KAJALA: Huwa naenda kumuona kila wiki.

HATAKI KUOLEWA TENA
Kajala miaka 12 mingi kwa mumeo jela, mimi nataka kukuoa. Msomaji, 0652672805
KAJALA: Hapana nimeolewa kanisani siwezi kuolewa tena.

YEYE NA SERENGETI BOYS
Kajala pole kwa masaibu ya jela, nimeshangazwa na tuhuma za wewe kujihusisha kimapenzi na ‘serengeti boys’ wakati mumeo unajua yupo gerezani, huoni kuwa unajivunjia heshima? Rocky, Moshi, 0715289337
KAJALA: Siyo kweli.

SHUKURANI ZIENDE KWA WEMA
Mshukuru sana Wema (Sepetu) kwani maisha ya jela siyo mazuri, angalia kazi na mwanaume usikurupuke tena. Msomaji, 0713361961
KAJALA: Wema ninamshukuru siku zote za maisha yangu, asante kwa ushauri.

HUYU ANAMJUA VIZURI
Mimi nakujua vizuri, tulisoma wote Chipole Songea, jina lako la shule ulikuwa unaitwa Winfrida Masanja, una mdogo wako anaitwa Doreen lakini baadaye ulihamia Jitegemee, naomba unitafute. Anthoni Kwass, Arusha, 0757154142
KAJALA: Ni kweli, nitakutafuta.

AMEACHANA KABISA NA P-FUNK?
Umepotea sana kwenye gemu, vipi mahakama haijakuruhusu kufanya kazi, na je, umeachana kabisa na P-Funk? Msomaji, 0769875335
KAJALA: Kazi ninafanya kama kawaida, P-Funk tulishaachana, ana mke tumebaki kumlea mtoto tu sasa.

ALIKUWA MAMALISHE?
Kajala wewe ni mwenyeji wa Mwanza, ulipotimkia Dar ulikuwa mamalishe na ulikuwa na mshikaji fulani kwa nia ya kuishi naye pande za Kigogo ila ulimtosa, je, ni kweli? Alex Kwanga, 0654066633
KAJALA: Siyo kweli, nimezaliwa Dar na kukulia hapahapa, Mwanza huwa naenda kuwasalimia bibi na babu tu.

AMEZALIWA MWAKA GANI?
Kajala umezaliwa mwaka gani na elimu yako umemaliza mwaka gani, filamu yako ya kwanza ni ipi, je, ni kweli ulighushi hela? Zaituni, Dar, 0659739717
KAJALA: Nimezaliwa mwaka 1983, nimemaliza kidato cha nne mwaka 1999, filamu yangu ya kwanza kushiriki ilikuwa inaitwa Lerato, kuhusu hela, mimi sikughushi kwa sababu sifanyi kazi benki.


Kwa hisani ya GPL

0 maoni: