Tuesday, 4 December 2012

Hili nalo neno.....

Jamani nahisi kushindwa kuvumilia hadi nahisi kufa na kishinda roho... najiuliza sipati jibu labda nikilileta hili jamvini linaweza likapata muafaka.... Hivi Zitto katoa wapi hela za kufanya private investigation Uswisi? Hivi mshahara na marupurupu yake yote kwa mwezi ni kiasi gani? Hivi ana biashara zipi alizo declare kama mbunge? all in all Zitto ana worth kiasi gani?

Sasa tujishajumuisha cha kujiuliza maswali yafuatayo:



1. Je kuna umuhimu gani yeye kwenda?

2. Je chama chake cha CHADEMA na uongozi wake wanalijua au wameshirikishwa?

3. Je Gharama za Hoteli, Chakula, Mawasiliano, Usafiri wa ndege na Taxi analipa nani? na  je zinaweza kufikia kiasi gani kwa siku?
4. Je serikali ya Uswisi inafahamu ujio wake na je watampa  ulinzi?
5. Je kaushirikisha Ubalozi wa Tanzania Geneva?
6. Je kaishirikisha Wizara ya mambo ya nje?
7. Je kaishirikisha Usalama wa Taifa
8. Je kaishirikisha wizara ya sheria?
9. Je kaishirikisha wizara ya utawala bora?
10.Je kaishirikisha OECD
11.Je kaishirikisha EU
12. Je kaishirikisha wizara ya fedha?
13. Je kaishirikisha BOT?
14. Je kazishirikisha hizo benki zilizofanya transfer?
15. Je kaishirikisha PCCB ?
16. Je kaishirikisha INTERPOOL?
17. Je kaishirikisha wizara ya fedha ya USWISI?
18. Je kaishirikisha BENKI KUU YA USWISI?
19. Je kaishirikisha POLISI YA USWISI?
20. Je kashawaandikia watuhumiwa barua za kujieleza? na alipoandika barua aliandika kama nani?
21. Je akikuta  hizo pesa zimehamisha na kupelekwa  nchi nyingine  ataendelea na ziara yake na kufanya uchunguzi zaidi?

22. Hivi wananchi wa jimbo lake wanazungumzia vipi hili swala  la mbunge wao kufanya ziara ya muda mrefu kwenye yenye matumizi makubwa wakati kuna vitu vinahitaji hela katika kutekeleza baadhi ya mambo kwenye jimbo lake?

Huyu ni mbunge kijana na mwenye kukubalika  ila  anapenda kujionyesha kuwa ana mawazo mbadala.Kama akitaka tumwone serious angeanza na TRA/TPA ili kujua kwa nini Tanzania inapoteza minimum BILIONI 300 kwa siku kutokana na uozo uliopo pale bandari na TRA na sio kuzidi kupoteza hela nyingi kwa kazi ambayo vyombo husika vingeweza kufanya

Zitto 2015 inakaribia jaribu kukaa chini na kufikiri haya yote........ tunakuhitaji kama kijana mwenye nguvu na kuweza kutoa hoja zinazoleta tija kwetu so usituboe na kutupa nafasi ya kukuchambua kama karanga ...........

Related Posts:

  • Barua ya Mwigamba yatua kwa msajili Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, imethibitisha kupokea barua ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba. Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya si… Read More
  • Sejusa: Museveni ajiandae kung'atuka Aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uganda UPDF, Generali David Sejusa(pichani) amezindua chama chake cha kisiasa nchini Uingereza na kumuonya Rais Yoweri Museveni kuwa utawala wake wa miaka 28 unaelekea ukingoni. Sejusa… Read More
  • Afande SELE kupambana na ABOOD? Msanii wa kizazi kipya, mfalme wa rymes, Selemani msindi a.k.a baba tunda, simba dume, AFANDE SELE (pichani) amesema sasa yupo tayari kwaajili ya mapambano ya kweli katika kuhakikisha jimbo la morogoro linapata kile wa… Read More
  • Hii ni fungua mwaka Read More
  • Shinawatra apona kuondolewa madarakani Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amepona kung'olewa madarakani baada ya kushinda kura ya kutokuwa na imani naye. Kumekuwa na maandamano siku kadhaa kutaka waziri mkuu huyo ajiuzulu kwa madai kwamba ni kib… Read More

0 maoni: