Saturday 15 December 2012

PETE ZA NDOA ZA MIKE, THEA ZAPOTEA KIMIUJIZA


SIKU chache kabla ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya ndoa yao, wasanii wa filamu Michael Sangu ‘Mike’ na mkewe Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ wamejikuta wakipoteza pete zao kimiujiza. Akizungumza kwa huzuni Mike alisema kuwa, yeye na mkewe Thea walitarajia kufanya sherehe hiyo Novemba 6, mwaka huu lakini hawakuweza kutokana na siku mbili kabla pete zao za ndoa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
“Yaani tumeshindwa kusherehekea miaka miwili ya ndoa yetu kwa sababu pete zimepotea kwenye mazingira ya ajabu sana. Zote zimepotelea bafuni, tena katika mazingira ambayo hatuyaelewi kabisa.“Tulichokifanya tumeenda kuchongesha pete nyingine na baada ya hapo tutazipeleka kwa mchungaji akaziombee kabla ya kufanya sherehe hiyo, tunajua haya ni majaribu ya shetani tu,” alisema Mike.

0 maoni: