Saturday 8 December 2012

PICHA YA SHARO YAMKOSESHA USINGIZI AMANDA

PICHA ambayo staa wa filamu Bongo, Tamrina Mohammed Poshi  ‘Amanda’ aliyoipiga na marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ inamkosesha usingizi kila akiitazama.Akizungumza Risasi hivi karibuni, Amanda alisema picha hiyo waliipiga wakati wa mwezi wa Ramadhani (Septemba, mwaka huu) ambapo Sharo Milionea alifunguka kuwa anatamani kufanya naye kazi, kweli wakafanya naye kazi ya pamoja katika mazingira ambayo hawezi kuyasahau.
“Mazingira ya yale mazungumzo yetu yanaponijia huwa nakosa usingizi kabisa. Tulifanya naye filamu ya Kitu Bomba ambayo haijatoka mpaka sasa lakini kwa kweli sasa hivi ananipa wakati mgumu sana, Mungu amlaze mahali pema peponi,” alisema Amanda.

0 maoni: