Saturday 8 December 2012

KAHABA AMTEGA ASKOFU


ASKOFU na Nabii, Nicolas Suguye wa Huduma ya Neno la Upatanisho (WRM), Matembele ya Pili, Kivule, Dar es Salaam amejikuta katika majaribu ya mapenzi baada ya msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Sharifa msomi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kummiminia meseji za kumtaka kimapenzi, Risasi Jumamosi lina kitu mkononi.
Akizungumza na paparazi wetu juzi jijini Dar es Salaam, msaidizi wa Nabii Suguye aliyejitambulisha kwa jina la Ruben alisema siku ya tukio mrembo huyo alipiga simu ya mtumishi wa Mungu ambayo alikuwa nayo yeye, akaipokea na kuanza kumtongoza.

“Siku hiyo huyo msichana alipiga simu ya huduma ya mtumishi nikaipokea mimi, yeye akaamini anaongea na Nabii Suguye, akajitambulisha yeye ni Sharifa, ni mwanafunzi wa UDOM, anatamani kuwa faragha na mtumishi siku hiyo.

“Aliniambia ‘nakupenda sana Nabii kwani nimekuwa nikifuatilia kipindi chako cha Matendo ya Nabii kupitia Runinga ya Sibuka. Hakika nakupenda sana naomba ukubali ombi langu la kuwa na wewe faragha, tafadhali.

“Huku akijua anaongea na Nabii Suguye, kahaba huyo aliniuliza niko wapi? Nikamjibu niko njiani kuelekea nyumbani, akasema nikifika nimjulishe. Nilipofika tu nyumbani, alipiga simu na kuniuliza kama nimefika, nikamjibu ndiyo.” alisema Ruben.

Ruben aliongeza kuwa, baada ya jibu hilo, Sharifa alimtaka aingie chumbani huku akimuuliza amevaa nguo gani siku hiyo?“Niliingia chumbani kweli huku nikimtajia nguo nilizovaa, nikashangaa ananiambia nivue nguo hizo zote na nilale kitandani ili anielekeze jinsi ya kufanya tendo la ngono na yeye,” alisema msaidizi huyo.

Alisema kitendo cha kuambiwa avue nguo kilimfanya amkemee msichana huyo huku akimwambia simu hiyo ni kwa ajili ya watu wanaohitaji huduma na si ya kuzungumzia mambo ya kijinga kisha mrembo huyo akatoweka hewani.

Juhudi za kumpata Nabii Suguye ili athibitishe madai ya tuhuma hizo zilifanikiwa ambapo  alikiri kupewa taarifa hizo na msaidizi wake na kukilaani kitendo hicho akisema  kikiendekezwa kinaweza kuua huduma za watumishi wa Mungu.

“Tukio hilo ni la kweli, tena napenda nitumie nafasi hii kulaani kwani kama Mtumishi wa Mungu hajasimama kiroho anaweza kuangukia mtegoni na kufanya zinaa,” alisema Nabii Suguye.

Kwa hisani ya - http://www.globalpublishers.info

0 maoni: