People's Magazine
The place where you can find everything...
Home
Saturday, 8 December 2012
Home
»
Celebrities News
,
Magazeti pendwa
» UKIMWI HUOO!
UKIMWI HUOO!
By
Unknown
21:41
No comments
KINACHOONEKANA kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa kubadilika na kuona ugonjwa huo ni wa kawaida kama ilivyo kukohoa au kichwa kugonga.
Hilo limedhihirika baada ya juzi chanzo chetu cha habari kupasha kwamba, baadhi ya wafanyabiashara na wabunge wameingia ‘kazi’ ya kuwanasa mastaa wa kike Bongo, hasa waigizaji wa filamu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wafanyabiashara maarufu wa jijini Dar na baadhi ya waheshimiwa wabunge wamekuwa wakiwaibukia mastaa wanapokuwa kambini wakirekodi filamu na kuwahonga fedha nyingi sanjari na kuwanunulia magari ya kifahari ya kutembelea.
MCHEZO UPO HIVI
Inadaiwa wanachofanya baadhi ya mastaa, hasa wakiwa kambini, hupiga picha chafu (angalia picha ukurasa wa mbele) wakiamini zina mvuto na kuzitundika BBM kwenye simu zao ambapo wafanyabiashara na wabunge hao wanapoziona huweweseka na kuanza msako wa kuwapata.
Chanzo kilisema: “Zamani mapedeshee ndiyo walikuwa wanaongoza kwa kuwachukua mastaa wa kike kwa kutumia picha za mitandaoni na kwenye magazeti, siku hizi mastaa wenyewe wamewashtukia, hawawataki mapedeshee, wanasema fedha zao ni za msimu.
“Siku hizi mastaa wakiwa kambini hupiga picha za hasarahasara na kuzitupia BBM, wafanyabiashara na wabunge wakiziona wanakimbilia kupanga foleni kwenye mahoteli ambayo mastaa hao wamepiga kambi.”
Aidha, chanzo kikasema kuwa baadhi ya wafanyabiashara huhonga kuanzia shilingi 1,000,000 hadi 5,000,000 kama staa ana jina kubwa.
“Kama staa ana jina kubwa, anaweza kuhongwa kuanzia milioni moja hadi tano, kama ni supastaa kama Wema, Wolper, Odama, Rose Ndauka hawa wanaweza kuhongwa hata magari ya kifahari,” kilisema chanzo hicho.
MASTAA WANAVYOTUMIKA
Chanzo kikasema kuwa, mbaya zaidi wanaume hao wamekuwa wakigoma kufanya mapenzi kwa kutumia kinga (kondom) kwa madai kwamba, hawawezi kuhonga pesa nyingi halafu kitandani wakatumia kondom kwani wanakosa raha.
“Kinachouma zaidi ni kwamba, hao wanaume wakiwachukua mastaa hadi chumbani wanakataa kutumia kondom, madai yao pesa wanazohonga ni ndefu (nyingi) kwa hiyo ni afadhali wafaidi, wanasahau kwamba Ukimwi upo.
“Kwa sababu ya tamaa ya pesa, dada zetu (mastaa) wanashindwa kuwa na msimamo wa kutumia kondom. Anaweza kukataa sana, lakini mheshimiwa anaahidi kumnunulia gari, hapo ndipo masharti yanalegezwa,” kilisema chanzo.
BAADA YA KUCHUJA KINACHOFUATA…
Chanzo kikasema kumekuwa na vilio na kusaga meno kwa baadhi ya mastaa kwani wanaponunuliwa magari, kadi zinakaa kwa wanaume hao, baadaye wanawanyang’anya.
“Mbaya zaidi, wapo mastaa waliwahi kushawishika na kutoa penzi bila kinga kwa ahadi ya kununuliwa gari, waliponunuliwa hawakupewa kadi ya kumiliki, baadaye wakanyang’anywa,” chanzo kilitoboa.
WASEMAVYO MASTAA
Baadhi ya mastaa waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwepo kwa wanaume wenye tabia hiyo, lakini kila mmoja akasema yeye haijamtokea.
Wolper: “Ni kweli, wapo wanaume wanabembeleza sana kutotumia kondom na kuahidi fedha au gari, lakini kama staa anakubaliana na ombi hilo ni kujiangamiza, Ukimwi unaua. Ila mimi sijawahi kukutana na mwanume wa hivyo, kwanza nilishasema ndani ya gari natembea na kondom.”
Jack wa Chuz: “Wewee, uamuzi wa kufanya hivyo ni wa mtu mwenyewe na umri wangu huu nikubali kufanya mapenzi bila kinga kwa sababu ya gari? Kwani gari kitu gani bwana.”
Nisha: “Mh! Nimewahi kusikia kuna wasanii waliingia kwenye mtego huo na sasa wanajuta maana hawana uhakika na afya zao, kwenda kupima wanaogopa, magari walishanyang’anywa, mimi aku!”
Flora Mvungi: “Mimi siwezi kusema kitu maana nina wangu, kama ni gari au pesa ananipa yeye, pole yao ambao hawajajipanga hadi leo.”
Aidha, chanzo kilisema kuwa, maeneo hatari ya kufanyika kwa michezo hiyo ni hoteli kubwa ambazo wasanii hupiga kambi kwa ajili ya kurekodi filamu.
Kwa hisani ya GLP
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Categories:
Celebrities News
,
Magazeti pendwa
← Newer Post
Older Post →
Home
0 maoni:
Post a Comment
Social Profiles
Popular
Tags
Blog Archives
Search this Blog
Jamani msiojua kuandika barua ya Uchumba deseni hapa .....
Mitindo ya nywele Wanawake wenye Rasta(dread)
Baada ya kufunga ndoa kimyakimya sasa Rais wa Masharobaro aitwa baba...
The face of El Salvador's gangs: 60,000 gang members on verge of war after court ruling threatens shaky truce between two warring factions
Members of both gangs hand over weapons and phones they were keeping illegally in Izalco prison as a means of maintaining the peace esta...
Kivazi hicho kazi kwenu
Wedding dresses for ladies
Unataka kuoa karibuni? hebu angalia suti za kisasa hapa ............
Man who found Internet fame when his skin turned permanently blue dies after suffering a heart attack
Paul Karason was 62 when he died Monday at Washington hospital He was admitted to the hospital after suffering a heart attack. He later ...
Wahamiaji Waafrika waandamana Israel
Maelfu ya wahamijai wa kiafrika, waliandamana mjini Tel Aviv Jumapili kupinga wanavyotendewa na serikali ya Israel. Waandamanaji hao wen...
Mwanamke mwenye HIPS kubwa kuliko wote huyu hapa ...
Curvy: Mikel Ruffinelli anapenda umbo lake na amekiri kuwa haoni sababu ya yeye kupungua, inasemekana hutumia kiti maalumu cha chuma mar...
Powered by
Blogger
.
My favorite News blog
Loading...
Celebrities Gossip
Loading...
.
Tags
Afya
(116)
Broken heart stories
(1)
Celebrities kids
(18)
Celebrities News
(783)
Children
(4)
Death Anouncement
(1)
Dini
(27)
Elimu
(5)
Extraordinary People
(12)
Familia
(26)
Full aibu
(87)
General
(20)
Karibu Jamvini
(1)
Katuni
(11)
Kazi za Jamii
(3)
Magazeti pendwa
(228)
Mahusiano
(281)
Majanga
(16)
mambo ya kuiga
(3)
Mapishi
(2)
Michezo na Burudani
(49)
Mikasa ya Maisha
(2)
Mila na desturi
(14)
Moyo Mpweke
(3)
Msaada kwenye tuta...
(10)
Nyumba
(28)
OMG
(476)
OMG... Black are beautiful
(10)
Picha huongea
(25)
Sayanzi na Tekinolojia
(3)
Siasa
(82)
Tangazo
(2)
Tiba Mbadala
(4)
True story
(77)
Ugaidi
(1)
Ukatili
(55)
umaarufu kazi
(28)
Urembo
(20)
Video
(10)
Vipaji
(3)
Vituko mtaani
(164)
Vivazi na Mitindo
(171)
Wanaume
(32)
Wanawake
(121)
0 maoni:
Post a Comment