Friday 14 December 2012

Mastaa wa kibongo kama wamerogwa?


MSANII wa filamu ambaye pia anafanya muziki, Zuena Mohammed  aka ‘Shilole’  na demu mwenzake aliyefahamika kwa jina la Hawa Juma ‘Mama Ayana’ hivi karibuni waliwaacha watu midomo wazi baada ya kugandana kimahaba mbele za watu. Tukio hilo lilitokea Msasani jijini Dar kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi ambako kulikuwa na pati ya kusherehekea kuzaliwa kwa Hawa.
Wakiwa eneo hilo, wawili hao walionekana kuwa karibu sana na lilipofika zoezi la kulishana keki na kufika zamu ya Shilole aliyekuwa MC, Hawa aliweka pembeni ‘stiki’ aliyokuwa akiitumia kulishia watu wengine kisha kutumia mdomo wake kumlisha msanii huyo.

Kitendo cha wawili hao kugandishiana midomo yao huku wakionekana wenye hisia, kilichukua muda wa takriban sekunde 60, mazingira yaliyowafanya baadhi ya waalikwa kuanza kunong’ona kuwa, kilichofanyika ni usagaji.

Angalizo
Jamani hawa  wanaojiita masupa staa wabongo hawawezi kufanya mambo ya kujega zaidi ya kuiga mambo ya ajabuajabu ?   sijui BASATA wanayaona haya au  wao wanaona kawaida? Nini maana ya kioo cha jamii?

0 maoni: