Friday 14 December 2012

Baby Madaha aumbuka! Adaiwa kodi ya nyumba ya miaka 3 ! apewa notice ya siku 2 ............

 
Wambeya wa mji tumezinyaka  taarifa za kusikitisha kuhusu msanii wa muziki wa kikazi kipya - tunda la Bongo Star Search Baby Madaha ....... Inasemekana Baby Madaha kapewa notice ya siku 2 na mwenye nyumba wake  na hii yote imetokana na msanii huyo kulimbikiza deni kwa muda wa miaka 3 kinachokadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 2 za kitanzania hadi sasa!!!


Nasikia Baby madaha kila siku alikuwa anampa  sound mwenye nyumba wake mara oooh nitakupa  kesho  mara wiki ijayo hali iliyomfanya mwenye nyumba huyo  kuchoka na kumpa notice ya siku 2 ili awe amelipa deni hilo.... kama haitoshi msanii huyo hajaonekana nyumbani hapo maeneo ya Kinondoni kwa siku tatu, na taarifa za notice katumiwa kwa njia ya kilongalonga - simu. 

Inasemekana Baba mwenye nyumba aligadhibika kinoma kiasi  cha kutaka kutoa vitu vya msanii huyo nje lakini kutokana na uvumilivu wake aliacha na aliamua kumpigia simu kuwa anampa siku mbili awe amelipa kiasi hicho cha pesa bila hivyo aondoe vitu vyake.
 


Wambeya hawakukubali wakavuta uzi na kumpata Baby  Madaha na alikuwa na haya ya kusema - Ni kweli taarifa za notice nimezipokea kwa njia ya simu ila hiyo habari ya  kutolala ndani ni ishu ya uongo! Baby aliongeza na kusema sijashindwa kulipa hela hizo lakini nilikuwa na mipango yangu naifanya kwani siwezi kudhalilishwa kwa pesa ndogo kiasi hicho hata kama anaishi kwenye nyumba ya kupanga.

0 maoni: