Thursday 13 December 2012

Hali hii Mbagala hadi lini?


 
Usafiri kwenye jiji hili la Bongo - Dar es salaam inaeleweka kabisa sio mzuri hasa majina ya asubuhi na jioni wakati watu wanaenda kutafuta riziki sehemu mbalimbali,  ila jamani wakazi wa Mbagala wamezidi....... Nahisi wenye mabasi nao wanawaendekeza bila kujali madhara gani yanaweza kutokea, hebu angalia hizi picha na ujiulize chanzo nini hasa? Hivi mwenye mabasi wakiacha hali hii iendelee mwisho wake ninini?  sasa kwa hali hii wanawake wangapi watapanda magari haya au kama watalazimisha kupanda mojamoja watajidhalilisha kwa kufanya nguo zao za ndani hata nyeti zao zibaki wazi..................... Nafikiri wakati umefika wa wenye mabasi kupiga mkwara na kuwapangisha foleni na watu waingie kiustaarabu ... hali hii kiukweli haipendezi....

0 maoni: