Sunday, 9 February 2014

Kifo cha Kanumba : Kesi kuanza kusikilizwa upya Februari 17

KAZI inaanza tena! Supastaa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anapanda katika kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania kwa yale madai ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa nyota wa muvi nchini, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Risasi Jumamosi limeambiwa. Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, mtoa habari ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema kuwa, Februari 17, mwaka huu, staa huyo atatakiwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kuanza huku akisema, kuna mabadiliko kidogo katika kusikilizwa kwa kesi hiyo.


ITAKUWAJE?
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, Lulu mwenye umri wa miaka 18, atasomewa upya mashitaka dhidi yake ambapo atatakiwa kujibu tena kama anakubali aliua bila kukusudia au la!
“Elizabeth (Lulu) atasomewa upya mashitaka ya kumuua Kanumba bila kukusudia. 
“Ataulizwa ni kweli au si kweli? Atatakiwa kujibu swali moja kati ya hayo mawili, kama ni kweli atasema kweli kama si kweli atasema si kweli,” kilisema chanzo hicho huku kikisisitiza jina lake lisichorwe gazetini.

MUDA WA KESI SIKU 730
Habari zaidi zikadondokea Dawati la Risasi Jumamosi na kusema kwamba, kesi hiyo itaendeshwa kwa siku mia saba na thelathini (730), kwa maana ya miaka miwili hadi hukumu itakapotolewa.

NI NDANI YA SHERIA MPYA
Katika Siku ya Sheria Duniani iliyoadhimishwa jijini Dar es Salaam, Februari 3, mwaka huu, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alisema kuanzia sasa kesi zote za jinai zitatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili.
Kesi ya Lulu nayo ni ya jinai na kwa sababu hiyo, hadi Februari ya mwaka 2016 itatakiwa iwe imemalizika.

WAKILI WAKE
Chanzo hicho kililithibitishia gazeti hili kwamba, Lulu atatetewa na yuleyule wakili wake mwenye ‘ngekewa’ ya kuwatetea watu maarufu nchini, Peter Kibatala.

Kibatala ameshawahi kuwa wakili wa Mbongo Fleva, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ katika kesi ya madai ya kuiba ‘power window’ za gari la msanii mwingine wa Bongo Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Pia aliwahi kumwakilisha wakili mwezake, Mabere Nyaucho Marando kwenye kesi ya Mbongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ alipoburuzwa kortini na uongozi wa Clouds Media Group baada ya Marando kuwa na udhuru.
Ilibaki kidogo awe wakili wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu katika kesi ya kumpiga makofi meneja wa hoteli moja (jina tunalo) iliyopo Kawe Beach, Godluck Kuyumbu lakini akakosa sifa baada ya shauri hilo kusiklizwa Mahakama ya Mwanzo Kawe, Dar.

HAWA HUENDA WAKAITWA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, katika kesi hiyo huenda wakaitwa watu ambao watasaidia kutoa ushahidi.
Watu hao ni wale waliokuwa na ukaribu na marehemu, hasa siku ya tukio au kushirikishwa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi ambavyo waendesha mashitaka wataona.

DOKTA KIDUME
Aliyekuwa akimtibu Kanumba, Dokta Kidume anaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ndiye aliyekuwa mtu wa pili  kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka.

SETH BOSCO
Huyu ni ‘mdogo’ wa marehemu Kanumba, yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja na marehemu, ila vyumba tofauti. Ndiye aliyemwona Kanumba akiwa katika hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia kumwita Dokta Kidume.  

Hawa wote walishahojiwa na Jeshi la Polisi Tanzania katika Kituo cha Oysterbay, Dar, mara baada ya kifo hicho. Seth alihojiwa mara tano.

TUJIKUMBUSHE
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam. Kifo chake kilidaiwa kilitokana na kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa na hivyo kuufanya ubongo kutikisika (brain concussion).

Hata hivyo, baadaye ilifahamika kuwa, sehemu ya maini na majimaji ya machoni vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kulikuwa na sumu au kitu kingine katika mwili wa Kanumba. Majibu hayajatoka hadi leo.

WAKILI KIBATALA
Risasi Jumamosi lilimsaka Wakili Kibatala kwa njia ya simu ili kumsikia alichonacho kufuatia kesi ya mteja wake kuanza kusikilizwa ambapo alisema:
“Tutakutana mahakamani jamani, kwa sasa niko bize sana.”

LULU
Juzi, simu ya Lulu ilipigwa kwa muda mrefu lakini haikupokelewa huku baadhi ya watu wake wa karibu wakisema kuwa, staa huyo ameasisi tabia mpya ya kutopokea simu zenye namba ngeni machoni mwake.

Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • Kimenuka! Kwa tukio hili, vijana wa mjini wanasema; kimenuka! Hivi karibuni wanawake watano ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja walinaswa usiku mnene wakifanya mapenzi na wanaume wawili kwenye chumba kimoja kilichopo Mw… Read More
  • Rose Ndauka anaswa kimahaba hadharani Staa anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke, Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio hilo lililoshuhudiwa na m… Read More
  • Hivi ndivyo alivyomkata mapanga mwanamke aliyezaa naye mtoto Vitendo vya kikatili vimekuwa vikitekelezwa katika sura mbalimbali, ila tukio la mtumishi wa Mungu, Padri Celestine John Nyaumba, 35, kumgonga kwa gari makusudi na kumcharanga mapanga mzazi mwenzake ni aibu isiyo na mf… Read More
  • LADY JAYDEE Vs Clouds MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, juzi Jumatatu hatimaye yalimkuta baada ya kuibua simanzi nzito katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, alipofikishwa baada ya kufunguliwa kesi ya madai namba 29/2013 na mabos… Read More
  • Mastaa wa KIBONGO na Pete za uchumba, Ndoa zimeishia ndotoni KATIKA ulimwengu huu kuna mambo mengi yanayofurahisha. Yapo pia yanayosikitisha na utapeli katika uhusiano wa kimapenzi umetamalaki. Nimeanza na utangulizi huo nikiwa na maana kuwa katika jamii inayotuzunguka inabidi… Read More

0 maoni: