Sunday, 19 January 2014

Skendo ya kukamatwa na Madawa ya Kulevya: Hatimaye Masogange amuanika hadharani mtu aliyemponza

HATIMAYE yule Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ aliyepatikana na hatia ya kuingiza nchini Afrika Kusini malighafi haramu aina ya ephedrine, amemtaja mtu aliyemtuma mzigo huo kuwa ni Mkongomani, Risasi Jumamosi limedondokewa na ‘kismati’. Katika mahojiano ‘spesho’ na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, juzi, Masogange aliamua kumwanika kigogo huyo huku akimtaja jina bila kuuma maneno.
TWENDE PAMOJA

Risasi: Masogange tumekuita leo hapa kwa ajili ya mahojiano maalum. Tangu umerudi Bongo toka Afrika Kusini ulikokutwa na ule msala wako, naamini hujawahi kuzungumza na chombo chochote cha habari. Uongo, kweli?
Masogange: Kweli kabisa.
Risasi: Risasi linakukaribisha tuzungumze mambo muhimu, lakini kubwa kuliko yote, hebu mtaje mtu aliyekutuma kubeba ule unga ambao ulikamatwa nao Afrika Kusini.
Masogange: (akionesha sura ya umakini) kusema ule ukweli, ni…(anamtaja jina). Huyu bwana ndiye aliyeniponza kwa yote yale.
Risasi: (bila mshtuko baada ya kutajwa kwa jina hilo). Huyo mtu ni Mtanzania kweli?
Masogange: Hapana, ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ila anaishi Tanzania miaka nenda, miaka rudi.
Risasi: Sasa Masogange, huyu mtu ilikuwajekuwaje hadi akakutuma kupeleka mzigo ule Afrika Kusini, hapo pana utata kidogo.
Masogange: Wengi hawajui. Iko hivi, siku ile (Julai 5, 2013) mimi nilikuwa nasafiri kwenda Sauz kwa mambo yangu tu. Nilipofika pale Uwanja wa Ndege (Julius Nyerere International Airpot) nilimkuta huyo mtu.
Risasi: Naye akiwa anasafiri kwenda huko?
Masogange: Hapana. Yeye tunafahamiana kwa muda mrefu, aliponiona aliniuliza kama nakwenda Sauz, nikamwambia ndiyo. Akasema anaomba nimbebee mizigo yake ya sukari.
Nilimkatalia, lakini akasema kuna mtu atanipokea Uwanja wa Ndege (wa Kimataifa wa Oliver Tambo) uliopo (Kempton Park) Johannesburg.
Basi nilimkubalia, lakini…
Risasi: Subiri kwanza Masogange.  Hapo una maana wewe kazi yako ilikuwa kubeba tu, baada ya kutua kule ungekutana na mwenye mzigo, Je, uliuangalia mzigo wenyewe kama kweli ni sukari?
Masogange: Ndiyo. Nilimwambia anifungulie nione kama kweli ni sukari, akafungua begi moja, nikachungulia na kuona kweli ni sukari nyeupe!
Nilimwambia kama anataka nimsaidie kuufikisha Afrika Kusini, apeleke mpaka kwenye ndege ili kunipunguzia kazi ya kubebabeba. Nikifika Sauz nitamtolea huyo mtu sukari yake.
Basi, akapeleka mpaka kwenye ndege, mimi nikapanda na safari ikaanza.
Risasi: Subiri kidogo Masogange. Wewe ulikamatwa na mtu anayedaiwa ni ndugu yako, Melisa Edward. Mbona humtaji?
Masogange: Oke, yule tulikuwa safari moja tu. Lakini yule Mkongomani anajuana na mimi.
Risasi: Oke, endelea.
Masogange: Tulifika uwanja wa ndege salama. Nikashuka na yale mabegi nayo, lakini cha ajabu wakatokea askari na kutukamata.
Waliniuliza nimebeba nini? Nikawaambia sukari, wakasema siyo sukari, wakanitaka nilambe. Kulamba hivi, ndiyo nikajua kweli siyo sukari, tukawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kwenye vyombo vyao vya sheria kwa hatua zaidi.
Risasi: Pole sana. Kwa hiyo yule mtu ambaye angepokea mzigo kule Sauz ulimwona ulipotua uwanjwa wa ndege?
Masogange: Sikuwa namjua kwa sura, nilipewa mawasiliano yake tu. Kuna uwezekano alituona wakati tumekamatwa na polisi maana tulizungukwa na watu wengi.
Risasi: Unakumbuka yalikuwa mabegi mangapi ya hiyo ‘sukari’? 
Masogange: Hata sikumbuki vizuri mimi, nilishachanganyikiwaga jamani, yalipita yale.


ANAYEMJUA MWAKYEMBE

Siku chache baada ya mlimbwende huyo kunaswa Sauz, Bongo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe alimtaja kijana ajulikanaye kwa jina moja la Mangunga kwamba ndiye aliyedaiwa kuwa na video queen huyo ndani ya ndege kwenda Afrika Kusini.


Mwakyembe aliamuru kijana huyo asakwe na kukamatwa ili kujibu mashitaka ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine kwa Tanzania huku Sauz ikisema ‘unga’ huo ni ephedrine ambao si wa kulevywa bali ni malighafi haramu.

Masogange na mwezake, Melisa walikamatwa Julai 5, mwaka jana kwenye uwanja huo wa ndege nchini humo wakiwa na madawa hayo yaliyokadiriwa kuwa na  thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Kesi yake iliendeshwa na Mahakama Kuu ya Gauteng iliyopo Kempton Park nchini humo na alikutwa na hatia ambapo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya randi 30,000 (shilingi milioni 4.8). Masogange alilipa faini huku mwenzake, Melisa akiachiwa huru kukutwa hana hatia.

Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • LEMA abaka? BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo (pichani) anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya … Read More
  • Mwizi wa kutumia bodaboda auawa KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa ni mzoefu wa wizi kwa kutumia usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada ya kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini. Tukio hilo … Read More
  • Namfuata MWISHO Namibia LICHA ya Mwisho Mwampamba kuwa mume wa ndoa wa Meryl Shikwambane, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amesema anajiandaa kwenda nchini Namibia wanapoishi wanandoa hao kwa lengo la kujumuika na Mwisho na kula ba… Read More
  • SHARUWA atoa waosia kwa Mastaa wa Kibongo KWENU, Wasanii mnaong’aa katika sanaa mbalimbali nchini. Ninafurahi kuwasiliana nanyi tena kwa wakati mmoja baada ya kuachana muda mrefu uliopita. Naamini mpo sawa na michakato ya kusaka mkate wa kila siku inaendelea vy… Read More
  • LADY JAYDEE Vs Clouds MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, juzi Jumatatu hatimaye yalimkuta baada ya kuibua simanzi nzito katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, alipofikishwa baada ya kufunguliwa kesi ya madai namba 29/2013 na mabos… Read More

0 maoni: