Thursday, 23 January 2014

Papa:Internet ni zawadi kutoka kwa Mungu

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki zao. Amewataka waumuni wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.
Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio nyaya tupu.
Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.
Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.
Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.
Chanzo - BBC Swahili

Related Posts:

  • Huu ndio Utajiri wa Marehemu Askofu KULOLA NI maswali tata yameibuka baada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evengelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk. Moses Samuel Kulola (85) kwamba, ameacha utajiri wa kiasi gani wakati wa uhai wake, Uwazi… Read More
  • Shehe PONDA awahenyesha POLISI masaa 24 HUWEZI kuacha kutafsiri kwamba, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anawahenyesha askari wa Dar es Salaam tena kwa saa 24, Ijumaa Wikienda limegundua. Hali hiyo imesababishwa na u… Read More
  • Mkorogo na Mtumishi wa Mungu inahusu? Jamani hivi vitu tuwe tunaangalia kabla hata hatujafanya! wenzetu walioendelea wanakuwa na watu wao wa kuwashauri baadhi ya mambo hata kama si makubwa basi madogo madogo kama haya ambayo yanaweza kuleta mushkeli mtaani...… Read More
  • Padri aliyemwagiwa Tindikali kusafirishwa Huenda Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, Anselmo Mwang’amba aliyemwagiwa tindikali siku tano zilizopita, akasafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kutokana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amba… Read More
  • RAY C aokoka? Read More

0 maoni: