Saturday 25 January 2014

Mapenzi ni noma......NISHA adaiwa kubembeleza penzi la Ney wa Mitego

STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kubembeleza penzi kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Ijumaa lina full mchongo. Mnyetishaji wetu alivujisha mawasiliano baina ya wawili hao waliowahi kuwa wapenzi kisha kumwagana ambapo yalionyesha kuwa Nisha analitamani upya penzi la staa huyo.

Mbali na mawasiliano ya ujumbe wa maandishi, chanzo hicho kilicho karibu na mastaa hao kilikwenda mbali zaidi kwa kuvujisha picha ambazo zilionesha Nisha akimtumia Nay huku akichombeza na meseji tofauti za kumtega.
Baada ya kuzinasa meseji hizo ambazo chanzo kilidai kimeziiba kutoka katika moja ya simu ya mastaa hao, paparazi wetu aliingia mzigoni kuwasaka mastaa hao ili kujua kama wana mpango wa kurudiana.
Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Nisha ambaye alisema: “Dah, ni kweli ninawasiliana na Nay kama rafiki wa kawaida tu.
“Nay ana demu wake na mimi nina bwana wangu.” 

Kwa upande wa Nay wa Mitego alipata kigugumizi kidogo kulizungumzia hilo lakini akakiri kupata meseji hizo za mitego lakini akadai hakuna kinachoendelea kati yao.

Kwa hisani ya GPL

0 maoni: