Saturday, 25 January 2014

Nicolas Anelka Matatani

Mchezaji wa soka wa timu ya taifa ya Ufaransa, Nicolas Anelka, anayeichezea klabu ya Westbrom amekanusha madai ya kufanya ishara inayoaminika kuwa ya kibaguzi dhidi ya Wayahudi. Anelka amesema atapinga vikali mashtaka dhidi yake ambayo huenda yakasababisha kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi yoyote ya soka ikiwa atapatikana na hatia.
Anelka, mwenye umri wa miaka 34, ameshutumiwa vikali kwa kufanya ishara hiyo, ambayo ilipigiwa debe sana na msanii wa Ufaransa Diedonne M'bala M'bala, ishara ambayo ilitajwa na wakosoaji kuwa ishara ya utawala wa Kinazi.
Mshambuliaji huyo wa Westbrom, amesema atapinga mashtaka hayo yaliyowasilishwa na Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza.
Ikiwa atapatikana na hatia Anelka huenda akakabidhiwa adhabu ya kutoshirika katika mechi tano mfululizo.
Klabu ya Westbrom halijasema lolote kuhusiana na mashtaka hayo ya FA, lakini imekariri kuwa Anelka ataendelea kuichezea klabu hiyo hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Kwa hisani ya BBC swahili

Related Posts:

  • Gwiji Gurumo ang’atuka 1940: Alizaliwa Kisarawe, Pwani  1960: Alianza muziki  Bendi alizopiga: Kili Chacha, Kilwa Jazz, Rufiji Jazz, DDC Mlimani, Safari Sound na Msondo Ngoma.   Alama na kielelezo cha muziki wa dansi nchini, m… Read More
  • Madawa ya Kulevya yamfilisi AISHA MADINDA WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetik… Read More
  • Malinzi achukua fomu ya urais TFF ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga SC, Jamal Malinzi amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu. Fomu hi… Read More
  • Kaseja akumbwa na balaa lingine! Rais Lupopo amuita paspoti yake yaibwa KIPA wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, ameendelea kukumbana na mikasa lukuki baada ya paspoti yake kuibwa katika hali ya utatanishi huku rais wa Klabu ya FC Lupopo, Victor Kasongo Ngoy, akimtaka aende DR Congo wiki hii.&nb… Read More
  • Yanga wamuongezea adhabu Mrisho Ngassa? IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, ndiyo iliyochangia ukubwa wa adhabu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Mrisho Ngassa, Championi Ijumaa limebaini. Taarifa hiyo inakuja wakati ambao Ngassa amefungiwa kucheza mechi sit… Read More

0 maoni: