Saturday, 11 January 2014

Gwajima avamiwa usiku na kunusurika kuuwawa

ILITOKEA lakini haikuandikwa kwa sababu haikudakwa! Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makazi yake kwenye Viwanja vya Tanganyika Perkas, Kawe jijini Dar, Josephat Gwajima alinusurika kuuawa mara tatu kufuatia kuvamiwa na majambazi watatu mwishoni mwa mwaka jana. Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, Gwajima alisema tukio hilo lilijiri nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar ambapo siku ya kwanza, majambazi hao waliingia nyumbani kwake saa nne usiku wakiwa wameficha sura na kumkuta yeye sebuleni ambapo walimuuliza, ‘Gwajima yuko wapi?’
“Ni kweli nilinusurika kifo na majambazi, walinivamia mara tatu nyumbani. Zilikuwa siku mbaya maishani mwangu. Siku ya kwanza walikuja na bunduki huku wameficha sura, walinikuta sebuleni, wakaniuliza alipo Gwajima, niliwajibu ametoka, wakaondoka wakisema watarudi kesho yake.
“Nilijua ni utani, lakini kweli siku iliyofuata saa nne usiku walikuja tena, wakanikuta ndiyo naingia nyumbani, wakaniambia niko chini ya ulinzi, nilimuomba Mungu aokoe maisha yangu kwani nilipatwa na mshtuko, wakahoji; ‘Gwajuma yuko wapi?’ Kabla sijajibu mmoja akasema; ‘huyu bwana mdogo ndiye tuliyemkuta jana,’ wakaondoka. “Sikuwa na wazo la kuripoti polisi ila nilimwamini Mungu aliye hai. Siku ya tatu walipitia juu ya paa kwa kung’oa vigae na kushukia chumbani wakiwa na bunduki.
“Mimi nilikuwa kitandani na mke wangu, wakauliza tena Gwajima yuko wapi? Nikawajibu bado hajarudi, wakasema; ‘haka (Gwajima) ndiyo kale kale ka bwana mdogo ka jana.’ “Mungu mkubwa, kwa nje zilisikika kelele za mbwa kisha wakatoweka ghafla, niliona ni siku za majaribu kwangu, nilimwomba Mungu atupilie mbali majaribu yale, baada ya siku kadhaa niliamua kuhama kwenye nyumba ile. “Ila nakumbuka ile siku ya mwisho walisema tunamtaka Gwajima kwa sababu anajifanya kufufua misukule kisha anataja majina yetu.
“Ndipo nilijua kumbe kisa ni kufufua misukule. Najua umbo langu ndiyo mkombozi wa yote kwani waliponiona walijua Gwajima hawezi kuwa na umbo dogo kama mimi nilivyo,” alisema Gwajima. Katika mahojiano marefu na gazeti hili, mchungaji huyo alisema kuwa mpango wa kumuua uliofanywa na mtu ambaye aliwahi kutajwa jina na binti msukule aliyemfufua kanisani kwake. Alisema mtu huyo aliyetajwa na msukule ni  mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (jina hakumtaja).


Kwa hisani ya GPL

Related Posts:

  • WEMA anaswa na Mwanaume TATA   STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amezua gumzo baada ya kunaswa akiwa katika  mikao ya ajabuajabu na mwanaume ‘tata’ maarufu kwa jina la Anti Bilal Mashauz.Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu Alhamis… Read More
  • JOHARI: SITEGEMEMI MABUZI KAMA MASTAA WENGINE   STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa hategemei wanaume kama wanavyofanya mastaa wengi wa kike Bongo.Akipiga stori na paparazi wetu  hivi karibuni jijini Dar, Johari amewataka… Read More
  • NGASSA akata Mzizi wa Fitina...... atua Mazoezini Yanga HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), amekata mzizi wa fitna baada ya kuanza kujifua rasmi na timu hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe. Awali kulikuwa na utata wa mchezaji huy… Read More
  • DOTNATA alishwa sumu? OOH my God! Mjasiriamali ambaye ni staa wa filamu na muziki Bongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ amedai kulishwa sumu kupitia juisi na kumsababisha hali yake kuwa mbaya, Amani lina taarifa kamili. Habari za uhakika zili… Read More
  • Wema Sepetu matatani tena? DIVA wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa h… Read More

0 maoni: