Monday, 27 January 2014

Ewura yafungia kituo pekee cha mafuta

Kituo cha kuuza mafuta wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, kimefungwa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (Ewura) hadi kitakapokamilisha ujenzi wa paa. Kwa mujibu wa barua ya Ewura ya Desemba 13 mwaka jana iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Miriam Mahanyu inakitaka kituo hicho kufungwa hadi kikamilishe ujenzi. Mkurugenzi wa kituo hicho, Rashid Nassoro alisema alipokea barua hiyo Januari 24 mwaka huu.
Nassoro aliomba Ewura kumruhusu kuendelea na huduma, huku akiendelea kukamilisha ujenzi. “Kwa kuwa agizo hili limekuja tukiwa na akiba ya mafuta ya mwezi mmoja,” alisema.
Baadhi ya wakazi wamelalamikia hatua hiyo, kutokana na kuwa kituo pekee kinachotoa huduma.
Kwa hisani ya Mwananchi

0 maoni: