Msimu wenye maridi kali kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani katika miongo miwli iliyopita, unaelekea kupiga maeneo ya Kusini na Mashariki mwa nchi hiyo. Miji ya New York na Washington ni miongoni mwa miji ambayo imekumbwa na theluji pamoja na baridi kali inayokuja kwa upepo mkali kutoka katika bahari ya Arctic.
Huku baridi ikizidi, gavana wa New York (Andrew Cuomo) amesema kuwa huenda baadhi ya barabara kuu zikafungwa.
Hali hii mbaya ya hewa imelazimisha kufungwa kwa shule huku biashara nyingi zikitatizika hata na safari za ndege pia zimekatizwa pakubwa.
Mamilioni ya watu wameonywa wasitoke nje.
Eneo lenye baridi kali ni Babbitt na Minessota. Theluji hiyo imesababishwa na hewa yenye baridi kali inayotoka katika bahari ya Arctic.
Angalia picha zaidi za tukio hili hapa chini
Habari na BBC Swahili
Picha na Mashirika
0 maoni:
Post a Comment