Monday 18 November 2013

Nani wa kulaumiwa hapa? Ndoa yangu ipo mashakani......

Naandika haya kwa masikitiko makubwa kwa hali iliyonitokea ijumaa ya juzi .Kuna mdada kazini kwangu imetokea kuzoeana sana kiasi kwamba lunch huwa tunakwenda pamoja huku tukiwa bega kwa bega .Tumezoeana sana kwa utani mwingi nwingi mpaka ananiitaga mume wake sweet darling licha ya kuona pete ya ndoa pale kidoleni.Kiukweli msg anazontumiaga huwa ni mbaya sana najitahidi kuzifuta kabla wife hajaziona.
Kipindi cha nyuma muda wa kazi ukiisha huwa anakuja kwenye gari langu tunabusiana kisha kila mmoja anashika njia yake..Sasa juzi usiku tukiwa na wife sebuleni huku nmmshika a new born baby boy wife alikua ameshika simu yangu sasa simu yangu ina mtindo wa msg kujifungua yenyewe nadhan ni settings ikaingia msg toka kwa bi mdada inasema hivi " helo swthrt micn u nipo kwa bed nakuwaza kesho plz twende escape 1 kuna kitu special 4 u.Kiukweli nilipata wakati mgumu sana kumuelewesha mke wangua jana jumamosi nmeshinda tu home nikifua nepi na kumbadilisha mtoto akijisaidia.Ingawa kwa macho anaonekana karidhika na utetezi wangu lakini bado namuona ana mashaka .Jamanu kina dada hata kama ni mazoea muwe munaangalia na muda wa kupiga simu au kutuma msg wengune tunawapenda wake zetu na tumetumia muda mrefu mpaka kuwatia ndani.

0 maoni: